WANANCHI WAMIMINIKA BANDA LA CHUO CHA SAYANSI ZA AFYA KOLANDOTO KUPIMA AFYA MAONESHO SHINYANGA

Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto kinachomilikiwa na Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) kilichopo katika Manispaa ya Shinyanga kimeshiriki Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga kwa kuonesha shughuli wanazofanya chuoni hapo, kutoa elimu ya afya pamoja na kutoa huduma kwa jamii  kwa kupima afya ikiwemo upimaji wa  Sukari, Shinikizo la damu na malaria.

Wananchi waliotembelea banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto  kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yaliyoanza Julai 23,2021 na kutarajiwa kuhitimishwa Agosti 1, 2021 katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga, wamechangamkia fursa zinazotolewa na chuo hicho ikiwa ni pamoja na kupima afya zao bure.

Akizungumza leo Ijumaa Julai 30,2021 , Mkuu wwa Idara ya Famasi katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Paschal Marusu amewahamasisha wananchi kutembelea banda lao ili wapime afya zao bure.

"Tunashiriki maonesho haya kwa kuonesha shughuli zetu za kawaida chuoni na aina ya mafunzo tunayotoa, tunatoa elimu ya afya pamoja na kutoa huduma kwa jamii za upimaji wa Sukari, Shinikizo la damu na kipimo cha haraka cha Malaria",amesema Marusu.

"Huduma hii ya upimaji afya bure katika banda letu ni Ofa maalumu katika kusherehekea Mahafali ya 9 kwenye Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto yatakayofanyika Siku ya Ijumaa Agosti 6,2021",ameongeza Marusu.

Marusu ametumia fursa hiyo kuwakaribisha watu wote wanaotaka kusoma mafunzo ya Sayansi za Afya katika kada za Nursing, Maabara, Utabibu, Famasia na Mafunzo ya Maabara Viwandani.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI 
Mkuu wwa Idara ya Famasi katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Paschal Marusu akizungumza kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga yanayofanyika katika uwanja wa Zainab Telack kijiji cha Butulwa kata ya Old Shinyanga Manispaa ya Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wwa Idara ya Famasi katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Paschal Marusu akizungumza kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. Kushoto ni Naibu Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Michael Henerco. Kulia ni Mteknolojia Maabara za Afya katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Daniel Makungu Shija.
Mteknolojia Maabara za Afya katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Daniel Makungu Shija akionesha kipimo cha haraka cha Malaria kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Kulia ni Muuguzi wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto,Peris Nderitu akionesha namna ya kumsaidia kupumua mtoto baada ya mama kujifungua halafu mtoto anashindwa kupumua kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.  
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Wananchi wakiwa nje ya banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Naibu Mkuu wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto, Michael Henerco na Muuguzi wa Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto,Peris Nderitu wakiwa kwenye banda la chuo chao kwenye Maonesho ya Biashara na Teknolojia ya Madini Shinyanga.
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Mwanafunzi wa Mwaka wa Tatu katika Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto akiwaonesha wanafunzi hatua za kufuata ukiwa unanawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni kwenye Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 
Shughuli za upimaji afya zikiendelea kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga.
Wanafunzi wakijifunza masuala ya afya kwenye banda la Chuo cha Sayansi za Afya Kolandoto katika Maonesho ya Pili ya Biashara na Teknolojia ya Madini Mkoa wa Shinyanga. 

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post