WALLACE KARIA APITISHWA KUWA MGOMBEA PEKEE WA URAIS TFF


Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) leo Juni 29, 2029 imempitisha Wallace Karia kuwa mgombea pekee wa nafasi ya Rais wa shirikisho hilo, baada ya kukidhi vigezo vyote.

Wallace Karia ambae ndio Rais wa sasa wa TFF jina lake pekee ndio lililopitishwa na kamati ya uchaguzi, baada ya wagombea wengine wa nafasi hiyo ya Urais Hawa Mniga pamoja na Evance Mgeusa kukosa vigezo vinavyokidhi kwa wao kuendelea na hatua inayofata kwenye uchaguzi.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF Benjamini Kalume amesema kwa sasa kitakachofanyika ni Wallace Karia akiwa kama mgombea pekee ni kwenda kuthibitishwa na Mkutano mkuu na si kumpigia Kura.

Mkutano Mkuu wa TFF utafanyika Agosti 7, 2021 Mkoani Tanga ambapo moja ya Ajenda ya mkutano huo ni Uchaguzi wa kuchagua viongozi wa shirikisho hilo ikiwemo nafasi ya Urais na nafasi sita (6) za wajumbe wa kamati ya Utendaji.
 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments