TAGCO YAAGIZWA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YA KIKAO KAZI CHA MAAFISA HABARI

Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza wakati wa kikao kazi cha Maafisa Habari



Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa  ameagiza Chama cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikalini kusimamia utekelezaji wa  Maazimio ya Kikao kazi kilichofanyika hivi karibuni Jijini Mbeya.

 Mhe.Bashungwa ametoa agizo hilo Juni 17, 2021 Jijini Dodoma alipukutana na kufanya mazungumzo na Viongozi wa Chama hicho ambao wamechaguliwa na Mkutano Mkuu wa Mwezi Mei 2021 Jijini Mbeya  kuongoza kwa muda wa miaka mitatu.

"Nawapongeza kwa kuchaguliwa, nasisitiza  mkatekeleze na kusimamia  majukumu yenu vyema, Mkurugenzi wa Idara ya Habari MAELEZO na  Msemaji mkuu wa Serikali pamoja na wasaidizi wake watakaa pamoja na nyinyi  mjadili maazimio ya mkutano ule kwa kina, mkakati wa namna ya kutekeleza pamoja na kuweka msisitizo unaohitajika"amesema Mhe.Bashungwa.

Kwa upande wake Pascal Shelutete amesema kuwa TAGCO ni moja ya kiungo muhimu katika kutoa habari za Serikali kwa jamii kupitia Maafisa Habari pamoja na kuisimamia vyema Kada hiyo muhimu kwa nchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments