RAWAN DAKIK ATEULIWA KUWA BALOZI WA HIARI WA MLIMA KILIMANJARO | MALUNDE 1 BLOG

Friday, June 11, 2021

RAWAN DAKIK ATEULIWA KUWA BALOZI WA HIARI WA MLIMA KILIMANJARO

  TANGA RAHA BLOG       Friday, June 11, 2021

 

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akimkabidhi zawadi ya picha Rawan Dakik (wa nne kutoka kushoto) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wake katika kutangaza Mlima Kilimanjaro, katika hafla fupi iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro . Mhe. Mary Masanja pia amemtangaza Rawan kama Balozi wa Hiari wa Mlima Kilimanjaro. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. John Mongella(wa nne kutoka kulia) wazazi wa Rawan, Mbunge wa Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Gambo(wa tatu kutoka kulia),Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhe.Jerry Muro (wa pili kutoka kulia) na Kaimu Mtendaji Mkuu wa TTB , Betrita Lyimo (kulia)

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kushoto) akimkabidhi ua Rawan Dakik (katikati) ikiwa ni ishara ya kumkaribisha baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro akitokea bara la Asia alikopanda Mlima Everest.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (kulia) akiteta jambo na wazazi wa Rawan kabla ya hafla fupi ya kumpokea iliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro. Mhe. Mary Masanja pia amemtangaza Rawan Dakik kama Balozi wa hiari wa Mlima Kilimanjaro.


Wizara ya Maliasili na Utalii imemteua Rawan Dakik kuwa balozi wa hiari wa Mlima Kilimanjaro ikiwa ni kutambua jitihada zake za kutangaza Mlima Kilimanjaro, baada ya kupanda mlima huo kwa takriban mara tano na pia kuipeperusha bendera ya Tanzania katika kilele cha mlima mrefu zaidi duniani Everest uliopo bara la Asia.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) ameyasema hayo leo wakati wa hafla fupi ya mapokezi ya Rawan Dakik yaliyofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mkoani Kilimanjaro leo.

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post