Marekani yazifunga tovuti za habari zenye mafungamano na Iran | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, June 23, 2021

Marekani yazifunga tovuti za habari zenye mafungamano na Iran

  Malunde       Wednesday, June 23, 2021


 Idara ya sheria ya Marekani imesema mamlaka nchini humo imezifungia tovuti za habari zenye mafungamano na serikali ya Iran kwa tuhuma za kueneza habari za upotoshaji.

Idara hiyo imesema tovuti 33 zilizofungiwa zilitumiwa na vituo vya redio na televisheni ya serikali ya Iran, vituo ambavyo serikali ya Marekani inavituhumu kwa kueneza habari za uwongo na zenye nia ya kuwapotosha wapiga kura wa Marekani kabla ya uchaguzi wa rais wa mwaka 2020.

Marekani imesema tovuti tatu kati ya hizo zilikuwa zinaendeshwa na kundi la Kata'ib Hizballah, ambalo zaidi ya muongo mmoja uliopita lilitajwa kuwa kundi la kigaidi.Kundi hilo ni tofauti na lile la wanamgambo wa Hezbollah ambalo tovuti zake za habari zinaendelea kufanya kazi.

Tangazo la Marekani linajiri saa chache tu baada ya shirika la habari la serikali ya Iran IRNA kusema, Marekani ilizifunga tovuti za Iran bila ya kutoa maelezo zaidi.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post