MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AWASILI NCHINI UFARANSA KUHUDHURIA JUKWAA LA KIZAZI CHENYE USAWA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, June 30, 2021

MAKAMU WA RAIS DKT.MPANGO AWASILI NCHINI UFARANSA KUHUDHURIA JUKWAA LA KIZAZI CHENYE USAWA

  Malunde       Wednesday, June 30, 2021


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango  Juni 29, 2021 amewasili  Paris nchini Ufaransa  ambako atahudhuria Jukwaa la Kizazi Chenye Usawa ( Generation Equality Forum) linalofanyika Paris Ufaransa kuanzia Juni 30 – Julai 2, 202.  Makamu wa Rais anamuwakilisha  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa hilo.

Aidha, Makamu wa Rais alipata maelezo jinsi Ubalozi wa Tnazania unavyotekeleza Sera ya Diplomasia ya Uchumi katika eneo lake uwakilishi ambalo ni Ufaransa,  Hispania; Ureno; Algeria na Morocco.   Maelezo hayo yalitolewa na Mhe. Samwel Shelukindo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa. Pia Balozi Shelukindo anaiwakilisha Tanzania katika Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)

Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango amempongeza Balozi Shelukindo kwa uwakilishi mzuri katika nchi hizo na kumuhakikishia serikali itaendelea kutatua changamoto zinazojitokeza katika ubalozi huo. Amemtaka kuendelea kutafuta mahusiano na sekta binafsi zilizopo nchini Ufaransa kwa manufaa ya nchi zote mbili. Hapo kesho juni 30,2021 Makamu wa Rais  anatarajia Kuhudhuria ufunguzi wa Jukwaa la kizazi cha usawa lenye lengo la kuchagiza haki za usawa wa kijinsia kama zilivyokubaliwa katika mkutano wa Beijing wa mwaka 1995.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post