Serikali Kuendelea Kuunga Mkono Kazi Za Sanaa


Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) wameahidi kuendelea kuunga mkono kazi mbalimbali za sanaa hapa nchini.

Hayo yamesememwa leo jijini Dar es Salaam na Afisa Sanaa Mwandamizi toka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Abel Ndaga wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya utoaji wa tuzo kwa wanafunzi wa vyuo wenye vipaji kupitia sanaa mbalimbali.

“Serikali kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wenye zamana na Sekta ya Sanaa kupitia BASATA tutaendelea kutoa ushirikiano na wasanii mbalimbali ili kuweza kufanikisha malengo ya kukuza sekta ya sanaa nchini.

Afisa Sanaa Mwandamizi Ndaga ameongeza kuwa kuelekea siku ya utoaji tuzo kwa wanafunzi wa vyuo wenye vipaji kupitia sanaa mbalimbali wanataraji kuwa tuzo hizo zitakuwa zitatoa hamasa kwa vijana wengi hapa nchini.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya utoaji tuzo kwa wanafunzi wa vyuo wenye vipaji kupitia sanaa mbalimbali  Joseph Ndalu ameahidi kuwa tuzo hizo zitaweka historia kwa kushirikisha wasanii wa tansia mbalimbali.

“Katika tuzo hizi tunatarajia kuwa na wasanii wa tasnia mbalimbali kama wasanii wafilamu, bongo fleva na sanaa mbalimbali hivyo ni imani yangu tuzo hizi zitakuwa za kipekee sana”alisema Bw. Ndalu.

Tuzo kwa wanafunzi wa vyuo wenye vipaji kupitia sanaa mbalimbali zitafanyika siku ya jumamosi Juai tatu katika Kituo cha Mikutano Cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja jioni.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments