MAJALIWA: SIMAMIENI MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA ZA SERIKALI


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka viongozi wa mkoa wa Dar es Salaam kusimamia ukusanyaji na matumizi sahihi ya mapato ili waweze  kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ametoa kauli hiyo jana (Ijumaa, Juni 4, 2021) alipozungumza na viongozi hao kwenye ofisi ndogo ya Waziri Mkuu Magogoni Jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa mbali na kusimamia ukusanyaji pia waweke mikakati ya kuwa na vyanzo vipya ambavyo vitasaidia kuongeza wigo wa ukusanyaji wa mapato "Tukishaongeza mapato haya, mabaraza yetu ya madiwani kwenye manispaa na jiji yanauwezo wa kupanga miradi inayoonekana  dhahiri na inayogusa maisha  ya wananchi "

Pia, Amesema kuwa mapato yanayopatikana kutoka kila chanzo  ni lazima matumizi yake yafanyike kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za matumizi ya fedha za Serikali.

Amesema kuwa viongozi hao wanapaswa kuweka mikakati itakayolifanya mkoa wa dar es salaam kuwa wakitalii badala ya kutegemea biashara pekee kama ilivyosasa "biashara ya utalii kwenye fukwe za bahari ya hindi inaweza kuwa chanzo kikubwa cha mapato katika mkoa wa Dar es salaam.

Kikao hicho pia kilihudhuriwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments