DKT. TULIA AWAOMBA WABUNGE KUIUNGA MKONO HOJA YA KUWA NA SIKU YA MWANAMKE MWENYE ULEMAVU


NAIBU Spika Dk.Tulia Ackson,akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Uchumi wa Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu nchini kilicho andaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kilichofanyika jijini Dodoma.

NAIBU Spika Dk.Tulia Ackson,akisisitiza jambo wakati wa  Mkutano Mkuu wa Uchumi wa Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu nchini kilicho andaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kilichofanyika jijini Dodoma.

Mshauri wa Bodi ya Ikupa Trust Fund ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum,Mhe. Stella Ikupa wakati wa  Mkutano Mkuu wa Uchumi wa Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu nchini kilicho andaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kilichofanyika jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Ikupa Trust na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchumi wa Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu nchini kilicho andaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kilichofanyika jijini Dodoma.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la kutoa msaada wa Kisheria nchini (LSF), Lulu Ng’wanakilala,,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchumi wa Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu nchini kilicho andaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kilichofanyika jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza,Aidan Eyakuze,akizungumza wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchumi wa Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu nchini kilicho andaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kilichofanyika jijini Dodoma.

Washiriki mbalimbali wakiwemo wadau wa watu wenye ulemavu na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakifuatilia mkutano wa pamoja uliowakutanisha ambao umeandaliwa na Mbunge wa Viti Maalum Stella Ikupa kupitia Taasisi ya Ikupa Trust jijini Dodoma.

Mshauri wa Bodi ya Ikupa Trust Fund ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum,Mhe. Stella Ikupa akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Mchinga (CCM) Mhe.Mama Salma Kikwete wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchumi wa Mapendekezo ya Siku ya Mwanamke Mwenye Ulemavu nchini kilicho andaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust Fund kilichofanyika jijini Dodoma.


Na.Alex Sonna,Dodoma

WABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameombwa kuunga mkono hoja ya kuwepo kwa maadhimisho ya siku ya mwanamke mwenye ulemavu.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson kwenye mkutano wa pamoja wa wadau wa Walemavu na Wabunge ulioandaliwa na Taasisi ya Ikupa Trust jijini Dodoma.

Akizungumza katika mkutano huo, Dk Tulia amewaomba Wabunge hao kuiunga mkono hoja hiyo pindi itakapoletwa bungeni na Mbunge wa Viti Maalum Stella Ikupa.

Naibu Spika Amesema uwepo wa siku ya mwanamke mwenye ulemavu itasaidia kuongeza wigo wa kujadili changamoto na matatizo wanayokumbana nayo wanawake wenye ulemavu nchini.

Dk Tulia amesema uwepo wa siku hiyo utatoa nafasi kubwa ya kujadili nafasi ya mwanamke mwenye ulemavu kwani kwa kipindi kirefu wamekua wakipata changamoto bila kuwa na sehemu ya kuziwasilishia.

” Ni kweli Walemavu wanakabiliwa na changamoto kubwa sana lakini wanawake wenye ulemavu changamoto zao ni kubwa zaidi, Kuna ambapo wanafanyiwa ukatili wa kimaumbile lakini hawawezi kujitetea, ni jukumu letu kama Wabunge kuipitisha hoja hii ili iweze kuwepo siku ya wanawake wenye ulemavu.

Niwaombe wabunge kuhakikisha kuwa hoja hiyo itakapoletwa bungeni iwe kwa kuletwa na Mbunge Stella Ikupa mwenyewe au hata Mbunge mwingine basi tuiunge mkono kwa asilimia 100, ili bunge liweze kuridhia, naamini Wabunge mmetuelewa,” Amesema Dk Tulia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi hiyo ya Ikupa Trust ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju amewaomba Wabunge hao kuipitisha siku hiyo kwa manufaa ya Watu wenye ulemavu.

“Hii hoja siyo yetu pekee yetu hata wenzetu wa shirika la kimataifa la Un Woman pamoja na shirika la idadi ya watu duniani UNFPA wametuunga mkono katika hili la kuwa na siku hii rasmi,” Amesema Mpanju.

Nae Mbunge Stella Ikupa amesema kupitia uwepo wa siku ya mwanamke mwenye ulemavu ni rahisi jamii kubadilisha mtazamo hasi dhidi ya watu wenye ulemavu na kuitumia pia siku hiyo kama sehemu ya kutoa Elimu kwa wananchi dhidi ya vitendo vyenye ukatili.

” Ni ombi langu kwenu Ndugu zetu Wabunge tutakapoileta hoja hii basi iweze kupita, tunaamini kuwa na siku moja Maalum ya wanawake wenye ulemavu kunaweza kusaidia kupunguza vitendo vya ukatili Kwenye jamii yetu,” Amesema Mhe. Ikupa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post