PROF. MKUMBO AITAKA FCC KUWEKA MAZINGIRA BORA YA UDHIBITI WA USHINDANI WA BIASHARA NCHINI

 

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo,akizungumza wakati akifungua Mkutano wa majadiliano ya Mpango Mkakati wa tano (5) wa FCC utakaoiwezesha Tume hiyo kuweka mazingira bora ya ushindani kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi uliofanyika jijini Dar es salaam.

Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua Mkutano wa majadiliano ya Mpango Mkakati wa tano (5) wa FCC utakaoiwezesha Tume hiyo kuweka mazingira bora ya ushindani kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi uliofanyika jijini Dar es salaam.


Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo ameitaka Tume ya Ushindani nchini - FCC kuweka mazingira bora ya udhibiti wa ushindani wa biashara nchini kwa lengo la kumlinda mlaji na bidhaa zinazozalishwa hapa nchini.

Prof. Mkumbo ametoa maelekezo hayo wakati akifungua mkutano wa majadiliano ya Mpango Mkakati wa tano (5) wa FCC utakaoiwezesha Tume hiyo kuweka mazingira bora ya ushindani kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi uliofanyika jijini Dar es salaam.

Aidha, ameipongeza FCC kwa kuandaa Mpango Mkakati unaoakisi Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Maono, Maelekezo na Mwelekeo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Sita.

Prof. Mkumbo pia amewatoa hofu wafanyabiashara kwa kusema kuwa Serikali kwa sasa haiendeshi shughuli za biashara kwa uhodhi wa dola bali kwa uhodhi wa sekta binafsi.

Amewahimiza wafanyabiashara na wamiliki wa Viwanda kufikiria na kuendesha shughuli zao kwa kuzingatia ushindani katika soko la Kijumuiya, Kikanda na Kimataifa kuliko kuangalia soko la ndani pekee.

Prof. Mkumbo pia ametoa wito kwa taasisi zote zenye jukumu la kuchangia FCC kufanya hivyo kwa wakati ili kuiwezesha taasisi hiyo kutekeleza majukumu yake ya msingi bila kukwama.

Naye, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe amesema FCC ina jukumu kubwa la kuhakikisha kuwa kuna ushindani wa bidhaa unaofuata misingi ya uhuru na haki katika soko huria huku ikidhibiti bidhaa hafifu na kumlinda mlaji kwa ajili ya uchumi shindani na maendeleo ya watu.

“ FCC ndio ina wajibu wa kuchagiza maendeleo ya viwanda yanayolenga kuwa na uchumi shindani unaotokana na bidhaa zilizoongezwa thamani na zenye ubora” Amesema Mhe. Kigahe.

Akiongea kabla ya ufunguzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tume ya ushindani (FCC) William Erio amesema mpango huo wa tano (5)tangu kuanzishwa kwa FCC unalenga kumlinda mlaji na kudhibiti bidhaa bandia ili kuleta ufanisi katika utendaji na kukidhi maarajio ya Serikali na wananchi kwa ujumla.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments