AKUTWA AMEFARIKI KWA KUPIGWA NJE YA DUKA LA VINYWAJI VIKALI



Mwili wa mwanaume anayedaiwa kuwa ni mfugaji mkazi wa kijiji cha Arirai wilayani Ngorongoro mkoa wa Arusha, Sabore Shumbi (44) umekutwa pembeni ya duka la kuuza vinywaji vikali katika kijiji cha Haydom wilaya ya Mbulu Mkoa wa Manyara ukiwa na majeraha kichwani kwa kupigwa na kitu chenye ncha kali.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Merrisone Mwakyoma amesema chanzo cha kifo hicho hakijajulikana akisema mwili huo umekutwa na majeraha matatu kichwani na kwamba watu waliokuwa wakipita eneo hilo ndio walioutambua mwili huo na kutoa taarifa polisi.

"Jina la mmiliki wa kibanda hicho linahifadhiwa wakati huu tunaoendelea na uchunguzi kwa sababu tangu kifo chake hakuna muuzaji wala mmiliki wa duka aliyeonekana wala kufungua duka",amesema Kamanda Mwakyoma



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments