WANAUME WAWILI WABADILISHANA WAKE ZAO KUMALIZA SKENDO YA UZINZI VICHAKANI

Wanaume wawili kutoka Uganda wameamua kubadilishana wake zao ili kumaliza sakata ya uzinzi kwa amani.

Hii ni baada ya mmoja wao Ali Mudde, mkazi wa kijiji cha Musoma katika kisiwa cha Jagozi kufahamishwa kuwa Bryan Masaba alikuwa anafanya mapenzi na mke wake katika kichaka kilichoko karibu.

Kwa mujibu wa Daily Monitor, Mudde akiwa na hasira za mkizi aliripoti suala hilo kwa mwenyekiti wa kijiji Peter Balikowa ambaye aliitisha kikao cha kutatua mzozo huo.

Ni wakati wa kikao hicho cha korti ya kijiji ndipo Balikowa aliwaagiza wanaume hao wawili kubadilishana wake zao iwapo wako sawa na bila kupoteza wakati wawili hao walikubali uamuzi huo.

"Sina pingamizi na uamuzi uliotolewa na mahakama hii na niko tayari kabisaa kumpa (Masaba) mke wangu," Mudde alisema.

Baada ya Mudde kukubali, mwenyekiti huyo alimuuliza mke wa Masaba iwapo yuko tayari kuwa na mke mwenza lakini alikataa katakata na badala yake kupendekeza kuwa mke wa Mudde.

Balikowa alikubali pendekezo hilo na kisha wanaume hao wawili walibadilishana wake zao bila tatizo.

Hakuna mwanandoa kati yao aliyekuwa na mtoto.

Katika tukio sawia na hilo lililoshudiwa nchini Kenya, wanawake wawili kutoka kaunti ya Busia waliwaacha wengi na bumbuwazi baada ya kubadilishana waume zao kwa lengo la kutafuta furaha.

Lilian Weta mwenye umri wa 28, mama wa watoto watatu na Millicent Auma mwenye umri wa miaka 29, mama wa watoto wawili walizua gumzo kwa kufanya jambo la lisilokuwa la kawaida. Wanawake hao wanadai walifanya uamuzi huo baada ya kusukumwa na sakata ya uzinzi usioisha katika familia zao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments