OLE SABAYA AFIKISHWA MAHAKAMANI | MALUNDE 1 BLOG

Friday, June 4, 2021

OLE SABAYA AFIKISHWA MAHAKAMANI

  Malunde       Friday, June 4, 2021


Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya akiwa na wenzake.

****

Leo Juni 4, 2021 aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wanne wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kujibu tuhuma zinazowakabili.

Hayo yanajiri ikiwa ni siku chache zimepita baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kumsimamisha kazi mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zinazomkabili.

Taarifa iliyotolewa Alhamisi ya Mei 13, 2021 na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa ilieleza kuwa, Sabaya alisimamishwa kazi kuanzia tarehe hiyo.

Rais Samia alichukua uamuzi huo ikiwa mheshimiwa Sabaya amehudumu katika nafasi hiyo kwa miaka michache tangu alipoteuliwa kuwa mkuu wa wilaya hiyo na Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli Julai 28, 2018.

Sabaya amefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi akiwa na walinzi wake sita na baada ya kushuka kwenye magari pamoja na wenzake walitakiwa kuchuchumaa kusubiri taratibu nyingine.

Baada ya muda mfupi walichukuliwa na kupelekwa katika chumba maalum wakisubiri kupelekwa mahakamani.

Kwa takribani wiki moja Sabaya alikuwa akihojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa tuhuma mbalimbali jijini Dar es Salaam.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post