Tanzia : MWIGIZAJI WA MIZENGWE MAARUFU MZEE MATATA AFARIKI DUNIA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, June 16, 2021

Tanzia : MWIGIZAJI WA MIZENGWE MAARUFU MZEE MATATA AFARIKI DUNIA

  Malunde       Wednesday, June 16, 2021

MWIGIZAJI wa Kikundi cha Maigizo cha Kashkashi kinachorusha mchezo wao wa kuchekesha wa Mizengwe kupitia Televisheni ya ITV, Jumanne Alela almaarufu Mzee Matata amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Juni 16, 2021 Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar alipokuwa amelazwa kwa matibabu toka Juni 13, 2021.

Taarifa ya kifo chake zimethibitishwa leo Jumatano Juni 16, 2021 na mkuu wa kitengo cha mawasiliano kwa umma Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Aminiel Aligaesha.

Aligaesha amesema msanii huyo amefariki dunia jana saa tano na nusu baada ya kulazwa katika hospitali hiyo tangu Juni 13, 2021.


Kwa mujibu wa mwigizaji maarufu nchini, @madebelidai, mazishi ya Mzee Matata yatafanyika kesho kwenye Makaburi ya Buguruni,Malapa jijini Dar es salaam.

“Mwanatasnia mwenzetu Mzee Jumanne Alela (Mzee Matata) yatafanyika kesho saa saba mchana kwenye Makaburi ya Buguruni-Malapa.


“Msiba upo kwa ndugu zake, Chamazi kwa Mkongo (jijini Dar),” taarifa kutoka kwa @madebelidai.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post