SHUJAA WA MAOMBI AFARIKI KWA KUGONGWA NA MTI WENYE MAPEPO | MALUNDE 1 BLOG

Monday, June 14, 2021

SHUJAA WA MAOMBI AFARIKI KWA KUGONGWA NA MTI WENYE MAPEPO

  Malunde       Monday, June 14, 2021


Shujaa wa maombi kutoka nchini Uganda Jimmy Obong, mwenye umri miaka 35 ameaga dunia baada ya kugongwa na mti unaoshukiwa kuwa na mapepo.

Jimmy Obong  amefariki dunia sikua ya Ijumaa wiki iliyopita akiwa pamoja na mashujaa wenzake wa maombi wakimuombea John Okodi katika kijiji cha Tecwao, Alebtong.

Ben Ogwang alikuwa ameandaa hafla ya maombi kwa jamaa yake mgonjwa aliyetambuliwa kama John Okodi, ambapo alimualika Jimmy Obong kuwa miongoni mwao wakiongozwa na Mchungaji Lawrence Ajuga.

Wakati wa maombi hayo mwanamke mmoja alipagawa na mapepo kisha akaanza kuwaelekeza watu katika mti ambao ulidaiwa kuwa na mapepo yanayohangaisha familia ya Okodi.

 Kisha baadaye waliamua kukata mti huo ambao ulimuangukia Jimmy Obong ambaye alifariki papo hapo.

Msemaji wa polisi katika eneo la Kyoga Kaskaizini, Jimmy Patrick Okema alisema wamewakamata watu 13 kufuatia kisa hicho akiongezea kuwa uchunguzi unaendelea.

"Ni kweli tumewakamata watu 13. Maafisa wetu wa polisi walitembelea eneo la tukio na mwili wa marehemu umepelekwa katika mochwari ya hospitali ya Alebtong Health Centre IV ukisubiri kufanyiwa upasuaji," alisema.Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post