WAZIRI UMMY AAGIZA WAKUU WA WILAYA WAAPISHWE KESHO JUMATATU, MZIGONI RASMI JUMATANO | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, June 20, 2021

WAZIRI UMMY AAGIZA WAKUU WA WILAYA WAAPISHWE KESHO JUMATATU, MZIGONI RASMI JUMATANO

  Malunde       Sunday, June 20, 2021

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tamisemi, Ummy Mwalimu ameagiza wakuu wa mikoa kuwaapisha Wakuu wa Wilaya wote walioteuliwa jana Jumamosi Juni 19,2021 na Rais wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuanzia kesho Jumatatu Juni 21, 2021 na endapo watachelewa sana basi wafanye Jumanne Juni 22,2021.

Waziri Ummy ametoa agizo hilo leo Jumapili Juni 20, 2021 muda mchache baada ya kumaliza ziara yake yake ya kukagua ujenzi wa stendi ya mabasi ya Mwenge jijini Dar es salaam.

"Kesho Jumatatu wote waanze mchakato wa kuwaapisha Wakuu hawa wa Wilaya. Kusiwe na kisingizio chochote, kama kuna sababu basi Jumanne mchakato huu ukamilike ili Jumatano waanze kazi mara moja",amesema.

“Waende wakaripoti kwenye vituo vyao vya kazi kwanza kisha baadaye warudi kwa ajili ya utaratibu wa kuhama. Wakuu wa Mikoa wote warudi kwenye vituo vyao vya kazi kwa ajili ya kuwaapisha Wakuu Wilaya wamechelewa sana basi wafanye Jumanne”, ameongeza Waziri Ummy.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy wakuu  wa wilaya walioteuliwa jana ni 139 kati yao 56 wapya na 83 wamebaki. kati ya 83 waliobaki, 26 wamebakishwa kwenye vituo vyao huku wengine wakihamishwa katika maeneo mbalimbali ili kuimarisha utendaji.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post