MADIWANI MANISPAA YA SHINYANGA WAKUTANA KUJADILI HOJA ZA CAG....DC MBONEKO ATAKA WAZEMBE WACHUKULIWE HATUA

 

Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye Baraza maalum la Madiwani Manispaa ya Shinyanga lililokuwa na Ajenda moja ya kujadili taarifa ya CAG na kufuta hoja zilizotolewa.
Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, wakipitia Makabrasha yenye taarifa za hoja za Mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za Serikali CAG.

Na Marco Maduhu, Shinyanga.

Madiwani wa Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga, wamejadili taarifa ya mkaguzi na Mdhibiti wa Hesabu za Serikali CAG, katika mwaka wa fedha 2019-2020.

Kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa hiyo ya CAG, kimefanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Manispaa hiyo ya Shinyanga ujulikanao kwa jina la Kalinjuna, huku kikihudhuriwa na watalaamu, viongozi wa siasa na baadhi ya wananchi.

Akisoma taarifa ya CAG kwenye baraza hilo maalum la madiwani Manispaa ya Shinyanga, Mweka Hazina wa Manispaa hiyo Nickson Itogoro, alisema kwa kipindi cha kuanzia Juni 30 mwaka 2020 Halmashauri hiyo imepata Hati Safi, lakini zimeibuliwa hoja 67.

Alisema kati ya hoja hizo 67, hoja 26 ni za kipindi cha nyuma, lakini hoja 41 ni za kipindi cha kuanzia Juni 30 mwaka jana, huku akibainisha kuwa mpaka sasa zimeshajibiwa hoja 25 na kubaki 42 ambazo bado zinaendelea kujibiwa.

Akizungumza kwenye baraza hilo, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, ameagiza wataalamu wa Manispaa ya Shinyanga ambao wamekuwa wakifanya kazi kwa uzembe na kusababisha kuwapo na hoja hizo za CAG wachukuliwe hatua.

“Hoja ambazo zimetolewa na CAG naziona kabisa zinatokana na uzembe, haiwezekani mtu unakaa na fedha za mapato ya Serikali mfukoni hata ndani ya mwezi mmoja na kutozipeleka Benki, pamoja na fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo kutopelekwa kwenye maeneo husika, huu ni uzembe,” alisema Mboneko,

“Ifike mahala watu ambao wanatusababishia hoja hizi za CAG wachukuliwe hatua, kwa sababu ukiangalia baadhi ya hoja zinajirudia rudia kila mwaka, na hili katika mwaka wa fedha ujao sitaki kuona linajirudia,”aliongeza.

Naye Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Serikali za mitaa Mkoani Shinyanga Alphonce Kasanji, alisema Siri ya mafanikio ya Halmashauri kupata Hati Safi ni kujibu hoja za CAG kwa wakati na kutokuwa na hoja nyingi, pamoja na Wataalamu kushirikiana kiutendaji na wakaguzi wa ndani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi, alisema katika hoja ambazo zimetolewa na CAG, Halmashauri hiyo ndiyo ina hoja chache, huku akiahidi kuyafanyia kazi maelekezo yote ambayo yametolewa kwenye baraza hilo.

Aidha Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila, amewataka pia wakuu wa Idara wa Manispaa hiyo wakae mguu sawa, kwa kuhakikisha wanatoa taarifa na kufuta hoja zote za CAG kila mmoja kwenye eneo lake.

Nao baadhi ya Madiwani wa Manispaa hiyo akiwemo Ezekiel Sabo wa Ibinzamata, walisema changamoto zote za kiutendaji ambazo zimejitokeza katika mwaka wa fedha 2019-2020, na kusababisha kuwapo na hoja hizo za CAG zifanyiwe kazi ili Halmashauri hiyo iendelee kulinda heshima yake ya kupata Hati Safi, na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa wananchi.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye Baraza maalum la Madiwani Manispaa ya Shinyanga lililokuwa na Ajenda moja ya kujadili taarifa ya CAG na kufuta hoja zilizotolewa.
Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Serikali za Mitaa Mkoa wa Shinyanga Alphonce Kasanji, akizungumza kwenye Baraza hilo maalumu la Madiwani Manispaa ya Shinyanga.
Meya wa Manispaa ya Shinyanga David Nkulila, akizungumza kwenye kikao cha Baraza maalum la madiwani.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga Geofrey Mwangulumbi akizungumza kwenye Baraza hilo.
Mwekahazina wa Manispaa ya Shinyanga Nickson Itogoro, akisoma taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa, kwenye Baraza Maalum la Madiwani.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga, wakiwa kwenye Baraza maalum la kujadili Taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga, wakiwa kwenye Baraza maalum la kujadili Taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga, wakiwa kwenye Baraza maalum la kujadili Taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa.
Madiwani wa Manispaa ya Shinyanga, wakiwa kwenye Baraza maalum la kujadili Taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa.
Wataalam wa manispaa ya Shinyanga ,wakiwa kwenye baraza la madiwani la kujadili taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa.
Wataalam wa manispaa ya Shinyanga ,wakiwa kwenye baraza la madiwani la kujadili taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa.
Wataalam wa manispaa ya Shinyanga ,wakiwa kwenye baraza la madiwani la kujadili taarifa ya CAG na hoja zilizotolewa .

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments