WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO KWA WIZARA YA HABARI KUHUSU SAKATA LA MECHI YA SIMBA NA YANGA KUAHIRISHWA


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kutoa taarifa juu ya sakata la mechi ya watani wa jadi timu za Simba na Yanga uliokuwa uchezwe katika Uwanja wa Mpira wa Mkapa jijini Dar es Salaam, juzi Jumamosi, Mei 8, 2021.

Kauli hiyo ameitoa leo May 10, 2021 baada ya kipindi cha kutambulisha wageni waliotembelea Bunge .

Amesema baada ya kuahirishwa wa mchezo wa watani wa jadi, Simba na Yanga uliotakiwa kuchezwa Mei 8 mwaka huu kulisababisha manung’uniko katika mitandao ya jamii lakini pia kutojua hatima ya waliolipa kiingilio katika mchezo hu

“Kufuatia kero hiyo, tayari tumeagiza Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuhakikisha wanatoa taarifa haraka sana kwa Watanzania mchezo wenyewe utachezwa lini lakini kuna viingilio ambavyo walikuwa wametoa hatma yake nini,” amesema.

Amesema wizara hiyo inatakiwa kutoa taarifa hiyo kwa kushirikiana na chombo kinachosimamia mchezo huo cha Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF).

Pia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewasihi Watanzania kuwa  wavumulivu ili kuipa muda Wizara kwa kushirikiana na taasisi zinazosimamia mpira wa miguu ikiwemo TFF kuja na taarifa juu ya hatima ya mchezo huo.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments