TMA YATOA TAARIFA KUHUSU MWELEKEO WA MVUA KWA SIKU KUMI ZIJAZO | MALUNDE 1 BLOG

Thursday, May 13, 2021

TMA YATOA TAARIFA KUHUSU MWELEKEO WA MVUA KWA SIKU KUMI ZIJAZO

  Malunde       Thursday, May 13, 2021


Kanda ya ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Shinyanga, Mwanza, Simiyu na Mara): Vipindi vya mvua na ngurumo za radi katika baadhi ya maeneo.

Nyanda za juu kaskazini-mashariki (Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro,): Vipindi vya mvua katika maeneo machache.

Pwani ya kaskazini (Mikoa ya Tanga, Maeneo ya kaskazini mwa Morogoro, Pwani na Dar es Salaam pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba): Vipindi vya mvua katika maeneo machache.

Magharibi mwa nchi (Mikoa ya Kigoma, Katavi na Tabora): Vipindi vya mvua zitakazoambatana na ngurumo za radi katika maeneo machache.

Kanda ya kati (Mikoa ya Dodoma na Singida): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla.

Nyanda za juu Kusini-magharibi (Mikoa ya Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla.

Pwani ya kusini (Mikoa ya Mtwara na Lindi): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla.

Kanda ya kusini (Mkoa wa Ruvuma na Maeneo ya kusini mwa Morogoro): Maeneo haya yanatarajiwa kuwa makavu kwa ujumla.

Imetolewana; MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIAUsikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post