MWILI WAFUKULIWA KABURINI, WAKATWA KICHWA , WANYOFOLEWA VIUNGO | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, May 25, 2021

MWILI WAFUKULIWA KABURINI, WAKATWA KICHWA , WANYOFOLEWA VIUNGO

  Malunde       Tuesday, May 25, 2021


Mkuu wa wilaya ya Gairo mkoani Morogoro, Siriel Mchembe ameagiza kutafutwa na kukamatwa kwa watu wanaotuhumiwa kunyofoa viungo vya mwili vya marehemu Rehema Michael Mei 24, mwaka huu.

Mchembe ametoa agizo hilo kwa jeshi la polisi wilayani humo, baada ya kubaini kuwa kaburi ulimozikwa mwili wa Rehema limefukuliwa na watu wasiojulikana, na kunyofolewa viungo kikiwemo kichwa, sehemu za siri, moyo na mapafu na kisha kutokomea navyo kusikojulikana.

Rehema alifariki dunia Mei 22 kwa ajali ya gari na kuzikwa katika kijiji cha Nguyami wilayani Gairo Mei 23 mkoani Morogoro.

Mchembe amefika kwenye kaburi hilo akiwa ameongozana na Kamanda wa polisi wa wilaya ya Gairo na Mganga Mkuu wa wilaya hiyo.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post