MASHINDANO MISS DODOMA 2021 YAZINDULIWA | MALUNDE 1 BLOG

Monday, May 10, 2021

MASHINDANO MISS DODOMA 2021 YAZINDULIWA

  Malunde       Monday, May 10, 2021


Na Faustine Gimu,Dodoma

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma Mlezi wa Mashindano hayo ya Miss  Dodoma na Morogoro  ambaye pia ni Mbunge wa viti  Maalumu Mkoa wa Morogoro Norah Waziri Mzeru  amesema kuwa jamii itambue Tasnia ya Urembo na Mitindo imekuwa chachu katika kujengewa mabinti uwezo wa kijasiriamali,kijamii na kiutamaduni.

Aidha,Mhe.Mzeru amewaomba viongozi mbalimbali na Taasisi binafsi na za kiserikali hususan  wabunge na wafanyabiashara kuwasaidia mabinti katika tasnia ya urembo na mitindo kuwapatia michango mbalimbali ili kuweza kuendeleza Tasnia ya urembo Nchini.

"Nikiwa kama mbunge wa viti maalumu mkoa wa morogoro katika Bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania nawaomba wabunge wenzangu kuchangia Tasnia  ya urembo na Mitindo kwani inatoa Ajira kwa mabinti zetu pamoja na kutangaza fursa mbalimbali za uwekezaji nchini",amesema .

Kwa upande wake  mkurugenzi wa NIKALEX LTD Alexander Nikitas ambae pia ni mwandaaji wa mashindano hayo amesema kuwa hii ni fursa kwa mabinti wa mkoa wa dodoma kujitokeza kwa wingi ili kushiriki mashindano haya ambayo yatawapa nafasi za kushiriki Miss Tanzania na  mshindi wa kwanza mpaka wa tatu ndiye atakayepata nafasi  ya kushiriki Miss Tanzania.

"Kabla ya Mashindano haya kufanyika ,Tarehe 21 mwezi wa 6 mwaka huu tutawakutanisha washiriki na  yatahusisha wilaya zote saba za Dodoma hivyo mabinti wote mnakaribishwa kushiriki mashindano haya"amesema Nikitas

Pia  Nikitas amesema jamii itambue kuwa tasnia ya urembo na mitindo  imekuwa chachu katika kuwajengea mabinti kuwa wana jamii wenye kutegemewa wawapo  katika mashindano haya.

Afisa Habari wa Mashindano hayo Ezekiel  Kwakwa amewahakikishia Wanadodoma na watanzania kwa ujumla kuwa mashindano hayo yatakuwa ya haki  na vigezo vyote vitazingatiwa na hakutakuwa na upendeleo wowote.
" Katika mashindano haya haki itatendeka hakuna upendeleo wowote utakaojitokeza"amesemaKwakwa.

Mashindano hayo yameshirikisha Warembo kutoka vyuo mbalimbali mkoani Dodoma na usaili unaendelea katika wilaya zote za Dodoma.

Mashindano ya Miss Dodoma yatahitimishwa Rasmi mwishoni mwa mwezi wa kumi mwaka huu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post