MAMLAKA ZA MAJI ZINAZOBAMBIKIZA BILI WANANCHI KUCHUKULIWA HATUA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, May 11, 2021

MAMLAKA ZA MAJI ZINAZOBAMBIKIZA BILI WANANCHI KUCHUKULIWA HATUA

  Malunde       Tuesday, May 11, 2021


Waziri wa Maji nchini Tanzania Jumaa Aweso amesema watazichukulia hatua mamlaka zote ambazo zitabainika kuwabambikizia bili wateja wa maji nchini.

Aweso ameyasema hayo jana Jumatatu Mei 10, 2021 wakati akijibu hoja zilizotolewa na wabunge wakati wakichangia makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaa wa fedha 2021/2022.

Alisema jukumu la wizara ni kuhakikisha kuwa mwananchi habambikiwi bili za maji

“Niwapongeze wabunge kwa kuwasilisha malalamiko ya wananchi wao,  hata mimi nilipopita huko nimesikia malalamiko hayo. Ni kweli anayelala na mgonjwa ndio anajua mihemo ya mgonjwa,” alisema.

Alisema baada ya kusikia malalamiko hayo wametoa maagizo kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma ya Maji na Nishati (Ewura) kufuatilia malalamiko hayo.

“Wameshafanyia kazi nataka niwadhibitishie wabunge mamlaka yoyote itakayokuwa imekwenda kinyume aidha kwa kuwabambikizia bili wateja au kutoa bili ambazo hazijaidhinishwa na Ewura tutazichukulia hatua hata ziwe na mapembe kiasi gani,” alisema.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post