WAZIRI AOMBA RADHI...SASA MECHI YA SIMBA SC Vs YANGA KUPANGWA UPYA...MASHABIKI KUPEWA TIKETI UPYA

Hatimaye Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imeweka wazi taarifa rasmi kuhusu sakata la kuahirishwa kwa mechi namba 208 ya Ligi Kuu Tanzania Bara (VPL) kati ya Watani wa Jadi Simba na Yanga iliyotakiwa kuchezwa Mei 8 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Bashungwa, amezitaka mamlaka za serikali zinazohusika na masuala ya tiketi kuhakikisha zinawapatia tiketi upya mashabiki takribani 43,000 waliokuwa wamekata tiketi.

Aidha ameagiza mamlaka za soka ikiwemo Bodi ya Ligi na TFF, kupanga upya tarehe ya mechi ya Simba SC vs Yanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post