WANAUME WAWILI WAKAMATWA WAKIIBA DAMU HOSPITALI - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Sunday, May 23, 2021

WANAUME WAWILI WAKAMATWA WAKIIBA DAMU HOSPITALI

Wanaume wawili wamekamatwa wakijaribu kuiba damu katika chumba cha upasuaji cha Hospitali ya Mafunzo ya Korle-Bu nchini Ghana.

Washukiwa hao wanaripotiwa kuingia katika chumba cha upasuaji cha hospitali hiyo mwendo wa saa nane asubuhi siku ya Jumamosi, Mei 23,2021.

Hata hivyo, walifumaniwa na mlinzi wa hospitali hiyo wakijitayarisha kusafirisha damu kupitia gari la Matiz.

Washukiwa hao wanaonyeshwa wakiwa na vifurushi vya damu mikononi mwao.

Taarifa kutoka kwa Hospitali ya Mafunzo ya Korle-Bu ilifichua kuwa wawili hao walikamatwa kwenye ghorofa ya tatu ya hospitali hiyo baada ya kudokezewa.

Taarifa hiyon iliongezea kuwa wawili hao wamepelekwa katika Kituo cha Polisi cha Korle-Bu kuhojiwa.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages