CAMILIUS WAMBURA ATEULIWA KUWA MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI (DCI) | MALUNDE 1 BLOG

Monday, May 31, 2021

CAMILIUS WAMBURA ATEULIWA KUWA MKURUGENZI WA UPELELEZI WA MAKOSA YA JINAI (DCI)

  Malunde       Monday, May 31, 2021

CP Camilius Wambura, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) mteule
 **
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amempandisha cheo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Camilius Wambura, na kuwa Kamishna wa Polisi (CP) ambapo pia amemteua kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI).

Taarifa ya uteuzi huo imetolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, na kueleza kuwa uteuzi huo umeanza jana Mei 30, 2021.

Mei 17, 2021, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, alimhamisha Wambura kutoka kuwa 'Chief of Operations Upel' kuu Dodoma na kumhamishia Dar es Salaam kuwa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum akichukua nafasi ya SACP Lazaro Mambosasa.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post