SIMBA SC YAIFUATA KAIZER CHIEFS AFRIKA KUSINI | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, May 11, 2021

SIMBA SC YAIFUATA KAIZER CHIEFS AFRIKA KUSINI

  Malunde       Tuesday, May 11, 2021Kikosi cha Simba SC

Klabu ya Simba SC itaondoka nchini leo Mei 11, 2021 kuelekea Afrika ya Kusini, kikosi hicho kitacheza mchezo wa klabu bingwa Afrika hatua ya robo fainali dhidi ya Kaizer Chiefs Mei 15, 2021.

Taarifa iliyotolewa na mabingwa hao wa Tanzania bara imeeleza,

''Kikosi cha mabingwa wa nchi kitaondoka alfajiri ya Jumanne Mei 11, 2021 (saa 9:45) kuelekea Afrika Kusini kupitia Kenya tayari kwa mchezo wa kwanza wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs utakaopigwa siku ya Jumamosi Mei 15, 2021''

Simba SC ilitinga hatua robo fainali baada ya kumaliza vinara wa kundi A wakiwa na alama 13 baada ya kushinda michezo 4 wametoka sare mchezo mmoja na walifungwa mchezo mmoja, Wekundu wa msimbazi walimaliza vinara wa kundi hilo mbele ya mabingwa watetezi Al Ahly ya Misri, AS Vital na AL Merrikh.

Na wanaanzia ugenini kutika mchezo huu kutokana na faida za kikanunu za kumaliza vinara wa kundi, kwa mujibu wa kanuni za CAF timu zinazomaliza kama vinara wa makundi zinapewa faida ya kuanzia ugenini na kumalizia nyumbani kwenye hatua ya robo fainali.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post