RAIS SAMIA AFUNGUA KIWANDA CHA USHONAJI CHA JESHI LA POLISI TANZANIA -KURASINI



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akivuta utepe kufungua Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi Tanzania kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam leo tarehe 18 Mei, 2021. Kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Khamis Hamza Khamis pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akimpongeza Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro mara baada ya kufungua Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi Tanzania kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam leo tarehe 18 Mei, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akipiga makofi na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Khamis Hamza Khamis pamoja na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya kukata utepe kuashiria ufunguzi wa Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi Tanzania kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam leo tarehe 18 Mei, 2021.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua kazi mbalimbali zinazofanywa katika kiwanda hicho cha ushonaji cha Jeshi la Polisi Tanzania kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam mara baada ya kukifungua leo tarehe 18 Mei, 2021
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua kazi za upimaji na ukataji wa vitambaa vinavyotumika katika kushona sare za Jeshi la Polisi katika Kiwanda cha Ushonaji Nguo cha Jeshi la Polisi Tanzania kilichopo Kurasini mkoani Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akikagua Gwaride la Heshima lililoandaliwa na Jeshi la Polisi Kurasini mkoani Dar es Salaam mara baada ya kufungua Kiwanda hicho cha Ushonaji
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Askari pamoja na Maafisa mbalimbali wa Jeshi la Polisi pamoja na Wageni wengine Kurasini mkoani Dar es Salaam mara baada ya kufungua Kiwanda cha Ushonaji cha Jeshi la Polisi Tanzania.

PICHA NA IKULU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments