FAMILIA YAPATA MSHTUKO WASIOJULIKANA KUWEKA JENEZA LENYE MAKOROKORO MLANGONI

 Familia katika kijiji cha Ebunyang'anyi kata ya Bunyala, Kakamega nchini Kenya imepatwa na mshtuko baada ya kuamka na kupata jeneza lililokuwa na misalaba mitatu likiwa limewekwa mlangoni  nje ya mlango wa nyumba ya Peter Wekondi, mzee mkongwe ambaye pia ni mgonjwa.

Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho cha kushangaza kilichotokea leo asubuhi, Janepher Masika amesema kuwa jeneza hilo lilikuwa limefungwa kwenye kitambaa cheupe huku nzi wakiwa wamejaa juu yake.

 "Leo asubuhi nilipokuwa nikienda shambani niliona jeneza nje ya nyumba ya majirani zangu na nikawaamsha kuwaarifu. Nilishtuka kwa sababu sijawahi kuona kitu kama hicho maishani," amesema Masika.

Kwa muda mfupi, tukio hilo lilikuwa limevuta umati mkubwa uliokusanyika katika boma hilo kushuhudia kisa hicho kilichowaacha midomo wazi.

Watu wasiojulikana walikuwa wameacha jeneza hilo nje ya mlango wa nyumba ya Peter Wekondi, mzee mkongwe ambaye pia ni mgonjwa .

Baada ya kufungua jeneza hilo wenyeji hao waliachwa na mshtuko baada ya kupata mchanga na vifaa vingine visivyojulikana. Baadhi yao walikihusisha kisa hicho na ushirikina ambao walisema huenda mhusika alichukua hatua hiyo kutokana na wivu. 

Jotham Makokha, mzee wa 'nyumba kumi' alitoa wito kwa wenyeji kupendana na kuishi kwa amani na uwiano. 

"Ninawarai watu wetu waachane na njia za kitamaduni zilizopitwa na wakati na kuleta hofu miongoni mwa wengi. Hatuishi tena kama enzi zile za mababu zetu", alisema Makokha.

 Familia ya waliotendewa kisha hicho yake Jackline Oteng'o sasa inaishi kwa hofu kubwa na sasa imetoa wito kwa yeyote aliye na habari kuhusu tukio hilo, kusaidia kutegua kitendawili kabla ya familia yake kuanza kushuhudia misururu ya maafa. 

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments