WAZIRI AWESO AZITAKA MAMLAKA ZA MAJI NCHINI KUACHA KUWAPA WASOMA MITA MALENGO MAKUBWA YA MAKUSANYO YASIYO HALISIA
Monday, April 26, 2021
NA MWANDISHI WETU, MWANZA.
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amewataka mameneja wa Mamlaka za Maji nchini kuwaeleza Mameneja Masoko wenu wasiwape wasoma mita malengo ya makubwa ya makusanyo yasiyo halisia ambayo hayatekelezeki na yanawaumiza wananchi na kusababisha malalamiko.
Badala yake aliwata mameneja hao wasimamie kikamilifu zoezi la usomaji wa mita za maji ziwe halisia ili kuepuka kuwabambikia wananchi bili za maji.
Aweso alisema hayo leo wakati wa ziara yake mkoani Mwanza ambapo alisema ni haki ya mwananchi kupatiwa huduma ya maji naye weajibu wake kulipa bili za maji lakini zisiwe bambikizi kwao.
Aliyasema hayo wakati akiwa kwenye mradi wa Maji wa Buswelo ambapo aliwaelekeza Mameneja Masoko hao kuhakikisha wanasimamia kikamilifu suala za usomaji wa mita za maji ili kuepusha malalamiko.
“Baadhi ya maeneo wananchi hulkalamikia bili za pemaji naomnba wakurugenzi waelekezei mameneja masoko wenu wasiwape malengo makubwa ya makusanyo wasoma mita yasiyohalisia maana leo unampa malengo makubwa ya makusanyo hafikii atakachokifanya atambamikizia bili mwananchi ili akuridhishe hivyo wekeni makarido halisia”Alisema .
Hata hivyo aliwataka wahakikisha wanaweka makadirio halisia juu ya kukusanya mapato ili wananchi waweze kulipa bili stahiki ambazo sio kichefuchefu.
Katika hatua nyengine amewataka Wakala wa Maji Vijijini Ruwasa na Mamlaka ya Maji ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mwanza kuhakikisha tenki lililopo eneo la Igogwe na kahama tokea 2017 ambalo hakuna usambaji wowote wa huduma maji wajipange miradi hiyo waende kuikamilisha na wananchi wapate huduma za maji.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundeblog@gmail.com
🚧🚦 Usiendeshe gari lako bila Mafunzo na Leseni halali_ 📲 Wasiliana nasi sasa: wa.me/255740273285 Unahitaji nini? 🚘 Unataka kujifunza udereva wa magari na kupata Cheti? 📄 Una cheti unataka kupata Leseni? 🔄 Unajua kuendesha lakini huna cheti wala leseni na unataka refresh upate cheti? 🛣️ Una nyaraka zote muhimu lakini unahitaji kujifua zaidi barabarani? ✅ Una Leseni bila cheti na unataka renew? 🌍 Tupo mikoa yote Tanzania hadi vijijini! 📞 Tupigie sasa: 0769 763 285
Social Plugin