WEZI WAVUNJA KANISA NA KUIBA NGUO ZA NDANI ZA PASTA

Waumini wa Kanisa la Makutano PAG eneo la Lurambi, Kakamega nchini Kenya wanahesabu hasara baada ya wezi kuvunja kanisa hilo na kuiba mali yenye thamani isiyojulikana. 

Kiongozi wa akina mama katika kanisa hilo Mama Prisca Orembo amesema walipata habari kuhusu tukio hilo Jumapili, Aprili 18,2021.

 “Tulifahamishwa kwamba kuna tukio kanisani na tulipofika hapo tulithibitisha ni kweli, wezi walivunja mlango wa kanisa na katika makazi ya mchungaji," Mama Prisca Orembo alinukuliwa na Citizen. 

Duru zinaarifu kwamba wezi hao waliiba mali kadhaa ikiwemo nguo za ndani za pasta na chakula chake jikoni.

 “Wezi hata wanaiba nguo za ndani za pasta wanaenda kuuza, hii ni nini?" alisema Wycliffe Sajida, ambaye ndiye pasta wa kanisa hilo.

 Pasta huyo alisema alipoteza kila kitu wakati wa kisa hicho.

“Walichukua suti mbili, mashati matano, viatu, mtungi wa gesi, nguo za kuhubiri na KSh. 2,500,” pasta Wycliffe alisema.

 Waumini wa kanisa hilo sasa wanataka idara ya polisi eneo hilo kuchukuwa hatua na kuwasaka wezi hao. 

CHANZO - TUKO NEWS

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments