VIJANA 854 WA JKT WALIOANDAMANA KWENDA IKULU WATIMULIWA | MALUNDE 1 BLOG

Sunday, April 18, 2021

VIJANA 854 WA JKT WALIOANDAMANA KWENDA IKULU WATIMULIWA

  Malunde       Sunday, April 18, 2021


Mkuu wa majeshi nchini Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo amesema vijana 854 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) waliokiuka taratibu kwa kuanzisha mgomo na kuandamana kwenda Ikulu wakishinikiza kuajiriwa jeshini  wamesitishiwa mikataba yao na kurudishwa majumbani.

Mabeyo ameeleza hayo jana Jumamosi Aprili 17, 2021 katika hafla ya kuwatunuku kamisheni maofisa wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) mjini Dodoma.

"Aprili 8,  2021 vijana wetu wa JKT wapatao 854 walianzisha mgomo,  kukataa kufanya kazi maeneo mengine  na kufanya maandamano kwenda Ikulu kwa madai ya kutaka kumuona rais ili wadai kuandikishwa jeshini kama walivyoahidiwa na aliyekuwa rais wa Tanzania,  John Magufuli."

"Vijana hao ni kati ya vijana 2400 walioahidiwa kuandikishwa jeshini na walifanya uamuzi huo baada ya jeshi kuamua kuwapunguza katika kazi ya ujenzi wa Ikulu Chamwino baada ya kazi kupungua ili waende kufanya kazi katika maeneo mengine lakini wao wakapinga kwa madai wangekosa kuandikishwa jeshini, " amesema Mabeyo.

Amebainisha kuwa jeshi halikuwa na lengo hilo na limelazimika kusitisha mikataba yao kwa kuwa kosa walilolifanya ni sawa na uasi na hauvumiliki.

Ameeleza kuwa pamoja na  kufanya uchunguzi  wa kwa nini walifanya hivyo,  jeshi limeamua kutafakari upya mpango wa kuchukua vijana wa kujitolea kwa ajili ya kujiunga na JKT.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post