PETER MSECHU AWACHANA WANAOMDHIHAKI MUONEKANO WAKE....ASISITIZA HIYO NI 'BRAND YAKE' | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, April 7, 2021

PETER MSECHU AWACHANA WANAOMDHIHAKI MUONEKANO WAKE....ASISITIZA HIYO NI 'BRAND YAKE'

  Malunde       Wednesday, April 7, 2021

Picha ya msanii Peter Msechu akiwa na mkewe aliyembeba mtoto wao
***
Msanii wa BongoFleva Peter Msechu amenyoosha maelezo kwa baadhi ya watu wanaomshambulia mitandaoni kuhusu muonekano wake kwa kusema hawezi kubadilika na hiyo ndiyo brand yake pia haimuathiri kwa chochote.

Kupitia EATV & EA Radio Digital Peter Msechu amesema "Hakuna kitu kinachoniathiri nitabakia kuwa Msechu na brand yangu itabaki hivi hivi na nitaendelea kuishi maisha yangu na kuzingatia kula vizuri, kuishi vizuri, kufanya mazoezi na sina magonjwa nyemelezi"

"Kuishi kama shabiki yangu anavyotaka yeye ili afurahi sitaweza ila shabiki ndiyo apende maisha yangu, kitakachoniuma ni watoto wangu wakishinda njaa, kukosa ada au familia yangu kutokuwa vizuri, napenda na nafurahi watu wafanye hivyo kwa sababu inafanya nizidi kuzungumziwa wala hainiumi" ameongeza Peter Msechu

Aidha msanii huyo amesema Mungu amemuumba kila mtu kwa mfano wake na aina yake ambayo anataka ayaishi hapa duniani.

Chanzo - EATV

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post