JENGO LA MOCHWARI LAPOROMOKA , MTU MMOJA AFARIKI, 11 WAJERUHIWA

 

Hifadhi ya maiti ya kaunti ya Vihiga nchini Kenya ambayo ilikuwa inajengwa iliporomoka na kumuua mwashi mmoja papo hapo na kuwaacha wengine 11 na majeraha mabaya. 

Lango la jengo hilo la kisasa lenye thamani ya mamilioni ya pesa liliporomoka Jumapili, Aprili 25,2021 mwendo wa saa tisa alasiri mjini Mbale. 

Kulingana na mkuu wa mawasiliano wa kaunti hiyo, waashi 38 hawakuwa wanafahamu hatari hiyo wakati walikuwa kwenye eneo la ujenzi. 

Waathiriwa 11 ambao walijeruhiwa walikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Vihiga huku mmoja akiwa katika hali mahututi. 

Mwili wa marehemu ulihifadhiwa kwenye makafani ya hospitali hiyo. 

Japo sababu ya kuporomoka kwa jengo hilo haijatajwa, wakazi wenye hamaki walidai kuwa ilitokana na msingi dhaifu na kuwaelekezea kidole cha lawama maafisa wa kaunti. 

"Msingi wa ujenzi huo ni mbovu na kushangaza endapo kandarasi hiyo ilipewa mhandisi," mmoja wa mashahidi alisema

 Jengo hilo lilizinduliwa na gavana wa kaunti hiyo Wilber Ottichilo, mnamo Februari 24,2021.

CHANZO- TUKO NEWS


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments