MGANGA MKUU WA SERIKALI ATAKIWA KUSIMAMIA MIFUMO YA UWAJIBIKAJI SEKTA YA AFYA NCHINI KUPUNGUZA VIFO VYA WAJAWAZITO | MALUNDE 1 BLOG

Saturday, April 10, 2021

MGANGA MKUU WA SERIKALI ATAKIWA KUSIMAMIA MIFUMO YA UWAJIBIKAJI SEKTA YA AFYA NCHINI KUPUNGUZA VIFO VYA WAJAWAZITO

  Malunde       Saturday, April 10, 2021


 Na WAMJW- Dom
Mganga Mkuu wa Serikali ametakiwa kusimamia mifumo ya uwajibikaji katika sekta ya afya nchini ili kupunguza vifo vya wajawazito pamoja na kupanua huduma za kibingwa ikiwemo vifaa vya kisasa ili kuvutia nchi za jirani kupata huduma za afya hapa nchini

Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Afya), Prof. Abel Makubi,  tarehe 9 Aprili,2021 wakati  akimkabidhi ofisi Mganga Mkuu wa Serikali  Dkt. Aifelo  Sichalwe kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Serikali  iliyopo katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Prof. Makubi ambaye alihudhumu nafasi ya Mganga Mkuu wa Serikali  hapo awali amempongez√† Dkt. Sichalwe kwa kuaminiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kuteuliwa kuwa Mganga Mkuu wa Serikali.

Aidha, Prof. Makubi amemtaka CMO huyo kusimamia  kusimamia suala la dawa, vifaa na vifaa tiba, kupambana na magonjwa yasiyoambukiza,  huduma za tiba asili,  ujenzi wa miundombinu pamoja na kusimamia mwenendo wa kuanza kwa Bima ya Afya kwa wote.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post