DANIEL CHONGOLO KATIBU MKUU MPYA WA CCM AKIMRITHI DKT. BASHIRU... SHAKA ACHUKUA MIKOBA YA HUMPHREY POLEPOLE


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amependekeza jina la aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Daniel Chongolo kuwa Katibu Mkuu wa Chama Mapinduzi na kushika nafasi ya aliyekuwa katibu Mkuu wa Chama hicho Dkt. Bashiru Ally.

Nafasi ya Katibu wa Itikadi na Uenezi iliyokuwa inashikiliwa na Humphrey Polepole imechukuliwa na Shaka Hamdu Shaka.

Shaka ambaye aliwahi kuwa Katibu Mkuu wa CCM mkoa wa Morogoro amepitishwa na Halmashauri Kuu Taifa ya Chama hicho, baada ya kupendekezwa na Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Christina Mndeme amepitishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuanzia leo Aprili 30, 2021.

Katibu wa Uchumi na Fedha Chama Cha Mapinduzi (CCM), Frank George Hawasi aendelee na nafasi yake, Katibu wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Ngebela Lubinga anaendelea na nafasi yake.

Katibu wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC) Oganaizesheni, Mama Maurdin Kastiko, ameshika nafasi ya Pereira Silima ambaye atapangiwa kazi nyingine ya kitaifa).

(Ndg Rodrick Mpogolo atapangiwa majukumu mengine ya kitaifa)

Naibu Katibu Mkuu Zanzibar Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Juma Sadala Mabodi nae anaendelea na nafasi yake ya awali.
Katibu Mkuu wa CCM, Daniel Chongolo
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi Taifa, Shaka Hamdu Shaka
Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Christina Mndeme


Mndeme anachukua nafasi iliyokuwa inashikwa na Lodrick Mpogolo, ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments