CAG ABAINI AKAUNTI YA JESHI LA ZIMAMOTO KUTUMIKA KUPITISHA SH261 MILIONI

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini kuwa akaunti ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji ilitumika kupitisha malipo batili ya shilingi milioni 261.

Akiwasilisha ripoti hiyo mbele ya waandishi wa habari mjini Dodoma leo, CAG, Charles Kichere amesema baada ya fedha hizo kuwekwa katika akaunti ya jeshi hilo halikutambua chanzo cha fedha hizo na hakukukuwa na mawasiliano na benki husika juu ya kupokea fedha hizo.

“Uongozi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji hazikutambua chanzo vya fedha hizo na hazikuwa na mawasiliano yaliyofanyika na benki kuhusiana na mapokezi ya fedha hizo.”amesema CAG, Kichere.

“Pia nilibaini kiasi cha fedha kilichukuliwa na mtunza fedha wa Zimamoto na uokoaji kutoka kwenye akaunti hiyo kwa kipindi tofauti kwa kutumia nyaraka za kughushi,”aliongeza.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments