Picha : RAIS SAMIA ASHIRIKI DUA MAALUM YA KUMUOMBEA HAYATI RAIS ABEID AMANI KARUME LEO ZANZIBAR


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiweka Shada la Maua katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume mara baada ya Dua iliyofanyika katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Zanzibar leo tarehe 07 April 2021 katika Siku ya Kumbukumbu ya (Karume Day)..PICHA NA IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiweka Shada la Maua katika Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume mara baada ya Dua iliyofanyika katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi (CCM) Kisiwandui Zanzibar leo tarehe 07 April 2021 katika Siku ya Kumbukumbu ya (Karume Day).


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Zanzibar Hussein Ali Mwinyi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, pamoja na Viongozi wengine wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakiomba Dua mbele ya Kaburi la Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar leo tarehe 07 April 2021 katika Siku ya Karume Day.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza jambo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa mara baada ya Dua Maalumu ya kumuombea Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume katika siku ya Kumbukumbu ya Karume (Karume Day) iliyofanyika leo tarehe 07 April 2021 katika Ofisi Kuu za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar.
Mhe Rais wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui mahali alipozikwa Hayati Rais Abeid Amani Karume Rais wa kwanza wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar , ambapo leo imefanyika Dua maalum ya kumuombea katika siku ya kumbukumbu yake.
Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mpinduzi Mhe Dkt.Hussein Ali Mwinyi akiwasili ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui mahali alipozikwa Hayati Rais Abeid Amani Karume,Rais wa kwanza wa serikali ya mapinduzi Zanzibar ambapo leo imefanyika Dua maalum ya kumuombea katika siku ya kumbukumbu yake.

Mhe rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki Dua maalumu ya kumuombea Hayati rais Abeid Amani Karume Rais wa kwanza wa serikali ya mapinduzi Zanzibar katika siku ya kumbukumbu yake. katika ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui mahali alipozikwa,leo April 7, 2021 .
Mhe Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Mjane wa Hayati Rais Abeid Aman Karume Mama Fatuma Karume , wakati alipowasili kwenye Dua maalumu ya kumuombea Hayati Rais Abeid Amani Karume,Rais wa kwanza wa serikali ya mapinduzi Zanzibar katika siku ya kumbukumbu yake. katika ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui mahali alipozikwa,leo April 7, 2021 .

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ,Mke wa Rais wa serikali ya Mapinduzi Zanziba Dkt. Hussein Ali Mwinyi , Mama Mariam Mwinyi, na Katibu mkuu Kiongozi wa serikali ya mapinduzi Zanzibar Mhandisi Zena Ahmed Said wakishiriki Dua maalumu ya kumuombea Hayati Rais Abeid Amani Karume,Rais wa kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika siku ya kumbukumbu yake, katika ofisi za Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui mahali alipozikwa, leo April 7, 2021 .

PICHA NA IKULU

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments