SAMIA : SIASA SI UADUI...USHINDI WA CCM 2025 UTATEGEMEA VILE TUTAKAVYOTEKELEZA ILANI YETU | MALUNDE 1 BLOG

Friday, April 30, 2021

SAMIA : SIASA SI UADUI...USHINDI WA CCM 2025 UTATEGEMEA VILE TUTAKAVYOTEKELEZA ILANI YETU

  Malunde       Friday, April 30, 2021

Mhe. Samia Suluhu Hassan

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema Ushindi wa CCM mwaka 2025 utaletwa kwa namna wana CCM watakavyotekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM huku akisisitiza kuwa Siasa si uadui hivyo kuviomba vyama vya siasa kutoa ushirikiano katika kuimarisha umoja uliopo.

Mhe. Samia ameyasema hayo leo Ijumaa Aprili 30,2021 wakati wa Mkutano Mkuu Maalum wa Chama Cha Mapinduzi uliofanyika mkoni Dodoma.

Amesisitiza kuwa kazi ya kukiimarisha Chama Cha Mapinduzi inaendelea huku akibainisha kuwa hatawaangusha wanawake na watanzania kwa ujumla.

Amesema licha ya kufahamu kazi aliyokabidhiwa siyo nyepesi lakini anaamini kwa uzoefu alionao anatosha na anaweza kuifanya kwa weledi na uwezo mkubwa na kwamba anazifahamu changamoto zinazowakabili watendaji wa ngazi za Mikoa na Wilaya

Mhe. Samia pia amesisitiza kusimamia maadili, kanuni na taratibu za chama hicho ili kuweza kufanya kazi kwa weledi katika kuwatumikia watanzania na wanachama wa CCM.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post