MSANII MMZY AACHIA ASCENT EP YENYE NYIMBO 8 KALI KUTIKISA ULIMWENGU | MALUNDE 1 BLOG

Monday, April 26, 2021

MSANII MMZY AACHIA ASCENT EP YENYE NYIMBO 8 KALI KUTIKISA ULIMWENGU

  Malunde       Monday, April 26, 2021
MMZY

Nyota anayekuja kwa kasi chini ya Lebo ya Kerae Records Akachukwu Emmanuel Uche maarufu kwa jina la MMZY ameachia rasmi EP yake ya kwanza iliyopewa jina la ASCENT EP yenye nyimbo 8.

Ni msanii ambaye anakuja vizuri kupitia Muziki aina ya Afrobeat akiwakilisha nchini Nigeria. Licha ya msanii huyu kuwa na ubora katika uandishi wake, sauti yake ni moja ya kitu kinachomtofautisha na wasanii wengine ambao wamewahi kutokea katika muziki nchini Nigeria.

MMZY ameachia rasmi EP yake ya kwanza iliyopewa jina la ASCENT EP yenye nyimbo 8 huku ikiwa na kolabo mbili akiwa ameshirikiana na msanii wa muziki Teni pamoja na Terri.

ASCENT EP imetayarishwa na watayarishaji watano ambaye ni Masterkraft,Echo The Guru,Cranker Mallo,Blaise Beats,Ozedikuz na nyimbo zote kukamilishwa na mtayarishaji Mix Monster.

Nyimbo zote zimeandikwa na msanii MMZY isipokuwa aliyoshirikiana na Teni pamoja na Terri na bila kusahau wimbo namba 3,4,5,8.

Dominate ni  wimbo wake unaofanya vizuri kwa sasa ukiwa unapatikana pia ndani ya EP yake hiyo iliyopewa jina la ASCENT.

Kuwa wa kwanza kusikiliza kazi zote kutoka kwenye EP kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo,apple music,boomplay,spotify,audiomack na youtube.

Kwa taarifa zaidi kuhusu MMZY unaweza kumfuata kupitia ukurasa wake wa Instagram @therealmmzy

Nyimbo Mpya za MMZY ni Medication, Dominate,Lies, Decale,Bum bum, Onye Egwu, Away aliyomshirikisha Ten na No Time aliyomshirikisha Terri. 

Sikiliza Nyimbo zote 👉<<HAPA>>

👇👇

 Mmzy Ascent

Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post