DKT. SUBI : TANZANIA TUPO VIZURI LAKINI TUSIBWETEKE TUENDELEE KUJIKINGA NA CORONA | MALUNDE 1 BLOG

Wednesday, April 14, 2021

DKT. SUBI : TANZANIA TUPO VIZURI LAKINI TUSIBWETEKE TUENDELEE KUJIKINGA NA CORONA

  Malunde       Wednesday, April 14, 2021


 Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Maendeleo ya Watoto, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.  Leonard Subi,akizungumza na washiriki wanaofanya tathmini ya mafanikio na changamoto katika utekelezaji wa kanuni za Afya za Kimataifa (International Health Regulations) katika kukabiliana na magonjwa ya mlipuko.

**

Mkurugenzi wa Huduma za Kinga kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,Wazee na Watoto Dk. Leonard Subi amesema kuwa Tanzania ni mojawapo kati ya nchi zinazochukua tahadhari kubwa sana ya kupambana na magonjwa ya milipuko kama Corona.

Aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha siku tatu kinachofanyika Jijini Arusha kilichoshirikisha wataalam mbalimbali, mashirika binafsi na wadau wa Afya  nchini.

"Tanzania tuko salama na wananchi wetu waendelee na maisha kama kawaida" alisema Dkt. Subi.

Vile vile Dkt. Subi ameendelea kusisitiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari zote za ugonjwa wa Corona ikiwemo utamaduni wa kunawa mikono kwa maji safi tiririka na sabuni, kuvaa barakoa kwa usahihi na kuepuka misongamano isiyo ya lazima. 

Aidha Dkt. Subi ametoa wito wa kuendelea kuyalinda makundi ya watu walio katika hatari ya kuathiriwa zaidi na ugonjwa wa Corona ikiwa ni makundi ya wazee pamoja na watu wenye magonjwa sugu kama Kisukari na presha.

Pia ameweka msisitizo kwa watanzania kuzingatia mtindo bora wa maisha ikiwa ni pamoja na kuzingatia mazoezi ya mwili na viungo na kuzingatia lishe bora ili kuongeza kinga za mwili katika kupambana maradhi ya kuambukiza pamoja na yale yasiyoambukiza.


Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post