Picha : KITUO CHA TAARIFA NA MAARIFA KILOLELI KISHAPU WAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI….WAANDAMANA KWENYE CHUMBA CHA KUJISTIRI WASICHANA

Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Kiloleli, Kwangu Limbu akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika leo Jumapili Machi 7,2021 katika shule ya Msingi Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kata ya Kiloleli Halmashauri ya wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga kimeadhimisha Siku ya Wanawake Duniani huku kikitoa hamasa kwa wanawake kubadilika na kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ili kufikia usawa wa kijinsia.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo Jumapili Machi 7,2021 katika shule ya Msingi Miyuguyu kata ya Kiloleli mahali ambapo Kituo cha Taarifa na Maarifa cha Kiloleli kinachosimamia na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) kilitoa hamasa kwa wananchi na wadau kujenga choo cha wasichana na chumba cha kujistiri kwa wanafunzi wa kike wanapokuwa katika hedhi.

Maadhimisho hayo ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8 ya TGNP kwa kushirikiana na wadau wake katika ngazi ya jamii na ngazi ya taifa ambapo TGNP imejipanga kufanya maadhimisho hayo kwa kipindi chote mwezi Machi, 2021 wakiongozwa na Kauli Mbiu ya kitaifa ambayo ni “Wanawake Katika Uongozi: Chachu kufikia Dunia yenye Usawa” na ujumbe mkubwa kutoka TGNP ni “Badili Mitazamo kuleta Usawa” lengo kuu ni kuangazia wanawake katika uongozi, ikiongozwa na msemo wa #ViongoziTuwaandaeSasa.

Maadhimisho ya Siku ya Wanawake duniani ngazi ya jamii yaliyoandaliwa na TGNP kupitia Vituo vya taarifa na maarifa  yamefadhiliwa na Kamesheni Kuu ya Watu wa Canada (Global Affairs Canada - GAC).

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kata ya Kiloleli, Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Kiloleli, Kwangu Limbu aliwataka wanawake kubadilika na kujitokeza kuwania nafasi za uongozi kwani wanawake wana sifa kama wanaume na wanazijua vyema changamoto zilizopo katika jamii zaidi ya wanaume.

“Wanawake tunatakiwa kuamka katika mfumo dume na mila na desturi kandamizi ambapo mwanamke anaonekana kuwa ni mtu wa kukaa tu nyumbani akimtegemea mwanaume. Wanawake simameni imara na muache kufikiria kuwa nyinyi ni wa nyumbani tu”,alisema Limbu.

“Wakati wa uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020 mimi nilidhubutu kuchukua fomu ya kugombea udiwani, nilipambana sana lakini changamoto niliyoiona ni wanaume wanawashabikia wagombea wa kiume na kuwaacha wanawake ambao kimsingi ndiyo wanazijua zaidi changamoto zilizopo katika jamii. Niwaombe wanawake wenzangu ukiona mwanamke mwenzako kajitokeza kuwania uongozi msaidie na mpe ushirikiano ili ashinde na hatimaye atatatua matatizo yaliyopo katika jamii”,aliongeza Limbu.

Aidha aliwasisitiza wanawake kutokubali kuachwa nyuma hivyo panapotokea nafasi za uongozi wajitokeze kuwania ili wapate nafasi ya kuongoza wananchi akibainisha kuwa mwanamke akipata uongozi ataweza kuwasemea wanawake na jamii kwa ujumla.

Mwenyekiti huyo wa kituo cha taarifa na maarifa pia alitumia fursa hiyo kuwashukuru wananchi na wadau mbalimbali waliojitokeza kujenga vyoo vya kisasa na vyumba vya kujistiri watoto wa kike katika shule ya msingi Miyuguyu ambapo sasa wanafunzi wanahudhuria masomo yao vizuri hata wakiwa katika hedhi.

“Tulitembelea shule ya Msingi Miyuguyu, kutokana na hali iliyokuwepo Wana Kituo cha taarifa na maarifa Kiloleli tulianza kuhamasisha jamii na wadau kuchangia ujenzi wa vyoo na chumba cha kujistiri watoto wa kike. Pia tumehamasisha ujenzi wa nyumba ya walimu katika shule ya msingi Mguda ambako pia choo na chumba maalumu kwa ajili ya watoto wa kike kujistiri kimjengwa. Tayari tumeona mabadiliko kwani utoro kwa watoto wa kike umepungua japo bado kuna changamoto ya ukosefu walimu wa kike kwani waliopo ni wa kiume tu”,alisema.

Kwa upande wake, Neema Jishiga ambaye pia mwaka 2020 alithubutu kugombea udiwani katika kata ya Kiloleli aliwataka wanawake kujikubali na kuepuka kukata tamaa kwani uongozi siyo mabavu na kila binadamu anaweza kuwa kiongozi huku akiwasihi wanawake kuacha kubeza wanawake wenzao wanaojitokeza kuomba nafasi za uongozi.

Akisoma taarifa kuhusu maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, mwana kituo cha taarifa na maarifa Kiloleli Eunice Keneja alisema maadhimisho hayo ni sehemu ya harakati za Ukombozi wa Wanawake Kimapinduzi, kwani kwa namna ya kipekee wanawake na wadau wanaotetea haki za wanawake huja pamoja kusherekea mafanikio waliyofikia, kutafakari changamoto zinazoendelea kuwakabili na kupanga mikakati ya jinsi ya kuzitatua kwa kutumia fursa zilizomo katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, vikundi na kitaifa.

Aidha alisema ufikiaji wa huduma za jamii bado ni changamoto hususani kwa wanawake kwani licha ya jitihada za kumtua mama ndoo kichwani bado vijijini wanawake wanatumia muda mwingi kutafuta maji na huduma za afya hasa afya ya uzazi.

Hata hivyo alieleza kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wanaishi katika ngzi ya vijini na kata na chimbuko la maendeleo ya nchi ni katika ngazi hiyo hivyo ushiriki mdogo wa wanawake katika nafasi hizo muhimu na za kimkakati ni bado ni changamoto katika kuleta usawa wa kijinsia na maendeleo jumuishi na endelevu akibainisha kuwa uwakilishi wa wanawake katika nafasi za uongozi wa kisiasa katika ngazi ya udiwani bado ni changamoto kubwa.

Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Miyuguyu Hamis Mashauri aliishukuru TGNP kupitia Vituo vya taarifa na maarifa kwa kazi nzuri inayofanya kwa kushirikiana na serikali katika kuhamasisha ujenzi wa vyoo na vyumba vya kujistiri watoto wa kike na masuala ya haki za wanawake huku akiwataka wanawake kujitokeza kwa wingi kuwania nafasi za uongozi.

Naye mkazi wa Kiloleli Martha Ngwelu aliwataka wanawake kuwa imara kuanzia ngazi ya familia hali itakayowafanya kujiamini zaidi na kuwa tayari kuomba nafasi za uongozi katika jamii huku Hellena Jidayi akiwasihi wazazi kukaa na watoto wao kike ili wajue changamoto wanazokutana nazo.

TGNP kwa kushirikiana na Vituo vya Taarifa na Maarifa katika Halmashauri 18 katika mikoa 9 nchini inafanya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa kipindi cha mwezi mzima (Machi) katika ngazi ya jamii ili kutambua na kusherekea wanawake walioleta mabadiliko na maendeleo katika maeneo yao.

 ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mwenyekiti wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Kiloleli, Kwangu Limbu akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika leo Jumapili Machi 7,2021 katika shule ya Msingi Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Neema Jishiga ambaye katika uchaguzi mkuu wa Tanzania mwaka 2020 alithubutu kugombea udiwani katika kata ya Kiloleli akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika leo Jumapili Machi 7,2021 katika shule ya Msingi Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Mwanakituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Kiloleli Eunice Keneja akisoma taarifa kuhusu Siku ya Wanawake Duniani wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika leo Jumapili Machi 7,2021 katika shule ya Msingi Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Wanawake wakicheza muziki wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika leo Jumapili Machi 7,2021 katika shule ya Msingi Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Wanawake wakicheza muziki wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika leo Jumapili Machi 7,2021 katika shule ya Msingi Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Wakazi wa Kiloleli wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika leo Jumapili Machi 7,2021 katika shule ya Msingi Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Wakazi wa Kiloleli wakiwa kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika leo Jumapili Machi 7,2021 katika shule ya Msingi Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Miyuguyu Hamis Mashauri akizungumza wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika leo Jumapili Machi 7,2021 katika shule ya Msingi Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Miyuguyu Hamis Mashauri (katikati) akiongoza Washiriki wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika leo Jumapili Machi 7,2021 kwenda kuona vyoo vipya na chumba cha kujistiri wanafunzi wa kike vilivyojengwa kutokana hamasa ya kituo cha taarifa na maarifa Kiloleli katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Miyuguyu Hamis Mashauri (mbele) akiongoza Washiriki wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika leo Jumapili Machi 7,2021 kwenda kuona vyoo vipya na chumba cha kujistiri wanafunzi wa kike vilivyojengwa kutokana hamasa ya kituo cha taarifa na maarifa Kiloleli katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Miyuguyu Hamis Mashauri (mbele) akiongoza Washiriki wa Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika leo Jumapili Machi 7,2021 kwenda kuona vyoo vipya na chumba cha kujistiri wanafunzi wa kike vilivyojengwa kutokana hamasa ya kituo cha taarifa na maarifa Kiloleli katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Miyuguyu Hamis Mashauri akionesha vyoo vipya na chumba cha kujistiri wanafunzi wa kike katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Kiloleli Zacharia Pimbi (kushoto) akielezea kuhusu chumba cha kujistiri wanafunzi wa kike katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Kiloleli Zacharia Pimbi (katikati) akielezea kuhusu chumba cha kujistiri wanafunzi wa kike katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Miyuguyu Hamis Mashauri akielezea kuhusu chumba cha kujistiri wanafunzi wa kike katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Katibu wa Kituo cha Taarifa na Maarifa kata ya Kiloleli Zacharia Pimbi akionesha choo cha wanafunzi wa kike katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Afisa Mtendaji wa kijiji cha Miyuguyu Hamis Mashauri akielezea kuhusu chumba maalumu kwa wanafunzi wenye ulemavu katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Miyuguyu Hamis Mashauri na Washiriki wa Maadhimisho ya Siku ya wanawake duniani wakiondoa baada ya kuona vyoo vipya na chumba cha kustiri wanafunzi wa kike vilivyojengwa kutokana hamasa ya kituo cha taarifa na maarifa Kiloleli katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Muonekano wa vyoo katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Muonekano wa vyoo katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Muonekano wa vyoo katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Muonekano wa vyoo vipya katika shule ya msingi Miyuguyu iliyopo katika kata ya Kiloleli wilayani Kishapu
Washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani wakipiga picha ya kumbukumbu katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga
Washiriki wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kata ya Kiloleli wakipiga picha ya kumbukumbu
Wananchi wakiwa katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Wananchi wakiwa katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Wananchi wakiwa katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Mkazi wa Kiloleli Martha  Ngwelu akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Hellena Jidayi akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Wananchi wakiwa katika shule ya Msingi Miyuguyu iliyopo katika Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Mjumbe wa serikali ya Kijiji cha Miyuguyu kata ya Kiloleli halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga akizungmza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Katibu wa Kituo cha Taarifa na maarifa kata ya Kiloleli, Zacharia Pimbi akizungumza na wanafunzi wa shule ya msingi Miyuguyu wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani
Katibu wa Kituo cha Taarifa na maarifa kata ya Kiloleli, Zacharia Pimbi akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake duniani

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments