AHUKUMIWA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA SIKU MOJA TU BAADA YA KUMUUA MME WAKE KWA PANGA | MALUNDE 1 BLOG

Tuesday, March 16, 2021

AHUKUMIWA KUTUMIKIA KIFUNGO CHA SIKU MOJA TU BAADA YA KUMUUA MME WAKE KWA PANGA

  Malunde       Tuesday, March 16, 2021

Picha Truphena Ndonga aliyemuua mumewe kwa panga
**
Mwanamke kutoka Kaunti ya Siaya nchini Kenya, Truphena Ndonga amefunguka kusema ameona miujiza wa ajabu ambao hakuutarajia baada ya kuhukumiwa kifungo cha siku moja kwa kosa la kumuua mumewe kwa Panga.

Truphena Ndonga amesema alijua maisha yake ndio yamefikia ukomo na alidhani angehukumiwa kifungo cha maisha au adhabu ya kunyongwa kutokana na kosa alilolifanya.

Akieleza chanzo cha kumuua mumewe James Oyengo kwa panga Truphena Ndonga amesema hakukusudia kufanya kitendo hicho ila mumewe alikuwa amelewa na kuanzisha ugomvi huku ameshika panga, hivyo akafanikiwa kujiteteta na kumpokonya panga mumewe kisha kumpiga nalo kama njia ya kujikinga.

Aidha ameendelea kusema kwa sasa anaishi kwa kaka yake na anaogopa kurudi nyumbani kwake kwani anajua uchungu wa upande wa ndugu wa mumewe haujaisha pia amepanga kuomba msamaha kwa familia ya mumewe.

Chanzo : Tuko News
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post