Picha : SHIRIKA LA THUBUTU LAENDESHA SHEREHE BOMBA ZA AKINA MAMA WILAYANI SHINYANGA


Meneja miradi kutoka Shirika la Thubutu Africa Intiatives (TAI) Paschalia Mbugani, akizungumza kwenye Sherehe bomba za akina mama wilayani Shinyanga zilizofanyika katika kata ya Didia kwa kukutanisha akina mama 50 kutoka Kata tatu za Nyida, Puni, na Itwangi.

Na Marco Maduhu, Shinyanga.

Shirika la Thubutu Africa Initiatives la mkoani Shinyanga, ambalo linatekeleza mradi wa USAID Tulonge afya limefanya sherehe bomba kwa aakina mama wenye watoto wa chinj ya miezi 6. Sherehe hizo ni moja ya shughuli za mradi wa USAID Tulonge afya unaohamasisha watu kubadili tabia zao za kiafya katika maeneo 5 ambayo ni afya ya mama na mtoto, afya ya uzazi, malaria, kifua kikuu na VVU/UKIMWI.

 Mradi huo unafadhiliwa na Shirika la misaada la watu wa Marekani (USAID) kupitia mashirika ya fhi360 na T-Marc Tanzania.

Sherehe hizo zimefanyika leo katika Kata ya Didia, na kuhudhuriwa na baadhi ya akina mama kutoka Kata ya Nyida, Puni, na Itwangi za Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga, zikiwa na lengo la kuwaleta akina mama pamoja ili kujadiliana masuala mbalimbali ya kiafya na kuwahamasisha kufuata tabia za kiafya katika malezi ya watoto wao ili kupunguza vifo vya watoto wa chini ya miaka 5. 

Tabia zinazohamasishwa ni pamoja na unyonyeshaji wa maziwa ya pekee kwa miezi 6 ya mwanzo, kulala kwenye chandarua chenye dawa kila siku, kufuata huduma za matibabu endapo ataona dalili za ugonjwa kwa mtoto, matumizi ya njia za kisasa za.afya ya uzazi ili kupishanisha watoto kwa angalau miezi 24 au zaidi na kukamilisha ratiba ya chanjo. Tabia hizo zinahamasushwa kupitia jukwaa la Naweza.

Akizungumza kwenye Sherehe hizo, Meneja miradi kutoka Shirika hilo la Thubutu Africa Initiatives, Paschalia Mbugani, amesema lengo la Sherehe hizo ni kujadiliana, kushirikishana uzoefu na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika kutekeleza tabia za kiafya na kushirikishana namna wanavyoweza kukabiliana na changamoto hizo. 

Sherehe hizo pia zimehudhuriwa na wataalamu afya ambao ni kaimu mganga mkuu, kaimu mratibu wa elimu ya afya kwa umma na kaimu mratibu wa afya ya uzazi na mtoto wote kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.

 Pia wauguzi waandamizi kutoka zahanati za Nyashimbi na Itwangi walikuwepo ili kuweza kutoa ufafanuzi wa kitaalamu na kujibu maswali ya washiriki kitaalamu.

"Tumekutana na akina mama hawa 50 kutoka kata Tatu za Nyida, Puni na Itwangi, kufanya Sherehe pamoja na majadiliano juu ya kuimarisha afya zao pamoja na watoto wao wale walio chini ya miezi sita, ambapo wanapaswa kuwa kwenye uangalizi wa hali ya juu ili kupunguza na hatimaye kumaliza kabisa tatizo la vifo vya watoto wa chini ya miaka 5.

 Kikubwa tunawahamasisha kuwanyonyesha watoto wao maziwa ya mama tu, bila ya kuwapa kitu chochote hata maji na nyingine”, amesema Mbugani.

Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga Peter Masanyiwa, amelipongeza Shirika hilo la Thubutu Africa Initiatives  kwa kazi nzuri ambayo wanayoifanya kwa kushirikiana na Serikali kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa akina mama, pamoja na malezi ya watoto na kuwataka akina mama hao kuifanyia kazi elimu ambayo wanapewa.

Pia amewaahidi akina mama hao kuwa, changamoto zote ambazo wanakabiliana nazo kwenye Sekta ya afya, Serikali itazifanyia kazi ili kuhakikisha wanapata huduma bora, na kuwasisitiza pale watoto wao wanapohisi ni wagonjwa wawawahishe hospitali kupata matibabu, na siyo kuwapeleka wakiwa na hali mbaya.

Aidha Kaimu Mratibu wa Afya ya Uzazi na Mtoto wilayani Shinyanga Regina Renatus, amewataka akina mama hao kufuata ushauri ambao wanapewa na wataalamu wa afya, ili kulinda afya zao na watoto wao.

Nao baadhi ya akina mama hao akiwemo Eva Juma kutoka kijiji cha Nduguti Kata ya Nyida, wametoa shukrani kwa elimu ambayo hua wanapewa na shirika hilo, ambayo imewasaidia kuokoa afya zao na watoto wao, ambapo walikuwa hawana elimu juu ya masuala ya afya ya uzazi, pamoja na unyonyeshaji sahihi kwa watoto waliochini ya umri wa miezi sita.

TAZAMA PICHA HAPA CHINI
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Peter Masanyiwa, akizungumza kwenye Sherehe bomba za akina mama wilayani Shinyanga zilizofanyika katika kata ya Didia kwa kukutanisha akina mama 50 kutoka Kata tatu za Nyida, Puni, na Itwangi.
Meneja miradi kutoka Shirika la Thubutu Afrika Intiatives, Paschalia Mbugani, akizungumza kwenye Sherehe bomba za akina mama wilayani Shinyanga zilizofanyika Kata ya Didia kwa kukutanisha akina mama 50 kutoka Kata tatu za Nyida, Puni, na Itwangi.
Msimamizi wa shughuli za mradi wa USAID Tulonge Afya mkoani Shinyanga Mugalula Jinai,akizungumza kwenye Sherehe bomba za akina mama wilayani Shinyanga zilizofanyika katika kata ya Didia kwa kukutanisha akina mama 50 kutoka Kata tatu za Nyida, Puni, na Itwangi.
Kaimu Mratibu wa afya ya uzazi mama na mtoto wilayani Shinyanga Regina Renatus, akizungumza kwenye Sherehe bomba za akina mama wilayani Shinyanga zilizofanyika katika kata ya Didia kwa kukutanisha akina mama 50 kutoka Kata tatu za Nyida, Puni, na Itwangi.
Mganga mfawidhi wa Zahanati ya Lyabukande Faustine Leonard, akizungumza kwenye sherehe hizo bomba za akina mama.
Teresia Bathoromeo, akitoa ushuhuda namna elimu ya afya ya uzazi, ili vyomsaidia kuimarisha afya yake na watoto wake.
Eva Juma, akichangia mjadala kwenye sherehe hiyo bomba za akina mama namna elimu ya afya ya uzazi ilivyosaidia kuokoa afya yake na watoto wake
Ester Daudi akichangia mjadala kwenye sherehe hiyo bomba za akina mama namna elimu ya afya ya uzazi ilivyosaidia kuokoa afya yake na watoto wake.
Mgeni Rasmi kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Peter Masanyiwa, akitoa zawadi ya Kitenge chenye ujumbe mbalimbali kwa akina mama hao, mara baada ya kumalizika kwa sherehe bomba.
Akina mama wakiwa kwenye sherehe yao, wakisikiliza elimu ya afya kutoka kwa wataalamu wa afya.
Sherehe zikiendelea.
Sherehe zikiendelea.
Sherehe zikiendelea.
Sherehe zikiendelea.
Sherehe zikiendelea.
Sherehe zikiendelea.
Sherehe zikiendelea.
Akina mama wakipiga picha ya kumbukumbu 

Na Marco Maduhu- Shinyanga.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post