JAMAA AMLA SAMAKI MWENYE THAMANI YA SHILINGI BILIONI 6


Picha ya jamaa aliyemvua samaki huyo
***
Unaambiwa usilolijua ni sawa na usiku wa giza na hilo limemtokea mvuvi mmoja huko nchini Nigeria aliyefahamika kwa jina la Zion Godwin ambaye amemvua samaki aina ya 'Blue Marlin Fish' mwenye thamani ya Tsh Bilioni 6 lakini amemla yeye na marafiki zake kijijini.

Taarifa hiyo imesambaa zaidi kwenye mitandao ya kijamii baada ya jamaa huyo kushea picha ambazo zilionesha akiwa ametoka baharini kumvua samaki huyo lakini kwa sababu ya kutojua thamani yake wakaamua kumfanya kitoweo.

Blue Marlin Fish ni moja ya aina kubwa za samaki duniani ambao wanapatikana katika bahari ya kitropiki kama Atlantic na Pacific tu, na kwa bara la Afrika wanapatikana zaidi kwenye nchi za Afrika Magharibi.

Aidha upatikanaji wao ni wa msimu hasa katika maeneo yenye joto na inasemekana ndani ya miili yao kuna aina ya madini ya Ruby na metali ya Zebaki ambayo matumizi yake ni kwenye mitambo na madawa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post