KAMPUNI YA TEMBO NICKEL YAANZA MIKAKATI KUJENGA KINU CHA KUCHENJUA MADINI YA NICKEL 'SMALTER' KAHAMA


Watu zaidi ya 1000 wanatarajia kuajiriwa katika kinu cha kuchenjua madini ya Nickel (Smalter ) kitakachojengwa katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi wilayani Kahama,mkoa wa Shinyanga katika uwekezaji wa kampuni ya madini ya Tembo Nickel.

Hayo yameelezwa jana na timu ya wataalamu wa serikali na muwekezaji wa kampuni ya kuchimba madini ya Nickel ya Tembo waliokuwa wilayani Kahama kuangalia maeneo ya kujenga mtambo ya kuchenjuwa madini hayo yatakayokuwa yanachimbwa toka kwenye wilaya ya Ngara mkoani Kagera.

Mtendaji mkuu wa kampuni ya Kabanga Nickel, Chris Showalter alisema uwekezaji wa ujenzi wa kinu hicho cha kuchenjua madini hayo utakapokamilika watu zaidi ya 1000 wanatarajia kuajiriwa katika Smalter hiyo itakayojengwa katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi katika halmashauri ya manispaa ya Kahama mji.

Showalter alisema pia katika uwekezaji huo kwa upande wa wilaya ya Ngara , mkoani Kagera watakapokuwa wanachimba madini hayo ya Nickel nako watu takribani 2000 wanatarajia kupata fursa ya ajira katika mgodi huo wa kampuni ya Tembo Nickel.

Awali akiongea kwenye kikao kabla ya kwenda kuangalia maeneo ya ujenzi wa Smelter hiyo, kamishina waTume ya madini nchini, Profesa Abdulkarimu Mruma aliyekuwa ameongoza timu ya wataalamu wa madini alisema serikali imetoa eneo la uwekezaji katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi, ili kurahisisha usafirishaji yatakapokuwa yamechejuliwa kwenye kinu hicho.

Profesa Mruma alisema ujenzi wa kinu hicho katika katika wilaya ya Kahama imependekezwa hapo kutokana kuwepo kwa uwekezaji wa migodi mikubwa ya dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi na utatumika pia kuchenjua makinikia ya dhahabu badala ya kusafirishwa nje ya nchi kazi yhiyo itafanyika hapa nchini katika Smalter hiyo.

Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack alisema serikali tayari ilishaandaa maeneo manne ya ujenzi wa mitambo ya kuchenjua madini ya Nickel na kutokana na fursa hiyo kumpeleka na kumuonyesha muwekezaji huo na wataalamu wake waweze kuchangua mojawapo watakalo ona panafaa.

Telack kutokana na fursa hiyo alimpongeza Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa busara yake katika kuamua ujenzi wa uwekezaji wa kinu hicho katika wilaya ya Kahama ambapo tayari serikali imeshaandaa maeneo ya ujenzi huo yanayokidhi mahitaji katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi manispaa ya Kahama mji.

Alisema serikali wilaya ya Kahama na mkoa wa Shinyanga wamepokea vizuri mradi huo na wataendelea kutoa ushirikiano wa karibu katika utekelezaji wa muwekezaji huo kwa maslahi mapana katika ukuaji wa uchumi wa taifa letu na kuitaka tume ya madini kufanya halaka kukamilisha taratibu ili ujenzi uanze mara moja.

Naye Meneja Mkuu wa Migodi ya Dhahabu ya Bulyanhulu na Buzwagi , Benedict Busunzu ameipongeza Kampuni ya Tembo Nickel ya kuchimba madini hayo kutoka Kabanga wilayani Ngara kwa kuamua kuwekeza kujenga kinu cha kuchenjua madini hayo eneo hilo na kuwa kampuni ya Barrick ipo tayari kukaa pamoja kuzungumza juu ya kutoa eneo uwekezaji huo.
Mkurugenzi wa kampuni ya kuchimba madini ya Nickel yanayopatikana wilayani Ngara mkoa wa Kagera akiongea na viongozi wa serikali mjini Kahama atakapojenga SMALTER ya kuchenjua madini hayo utakao jengwa katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi wilayani Kahama .
Muwekezaji wa kujenga Smalter ya kuchenjua madini ya Nickel alipotembelea maeneo ya kujenga mitambo hiyo katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi

Mtendaji mkuu wa kampuni ya Tembo Nickel ya kuchimba madini ya hayo akiongea mbele ya kamishina wa tume ya madini nchini Profesa Abdulkarimu Mruma na mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack kwenye kikao cha pamoja na wataalaamu wa madini wa serikali na muwekezaji huyo kilichofanyika mjini Kahama alipokuja kuangalia eneo la kujenga mitambo ya kuchenjua madini hayo utakaojengwa katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi.
Mwekezaji wa kampuni ya kuchimba madini ya Nickel ya Tembo Nickel , Chris Showalter aliyekaa wa kwanza akiwa kwenye kikao na wataalamu wa madini pamoja na viongozi wa serikali wa wilaya ya mkoa wa Shinyanga .
Kamishina wa tume ya madini nchini ,Profesa Abdulkarimu Mruma akionyesha katika kikao na muwekezaji andiko la mapendekezo katika mradi wa ujenzi wa kinu cha kuchenjua madini ya Nickel (SMALTER ) itakayojengwa katika mgodi wa dhahabu wa Buzwagi ambapo madini hayo yanachimbwa katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera kulia ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post