JITIBU MWENYEWE KWA TIBA HIZI ZA NYUMBANI


Vyakula vinavyoweza kukupatia nguvu mwilini ili kujenga kinga yako na kudhibiti magonjwa
 ***
Wakati mwingine umeziskia hizi tiba za nyumbani ili kutuliza maumivu ya kichwa na hata kuweza kupata usingizi.

Mara nyingi tiba hizi umezipata kwa wazee wetu wa zamani ama hata kuzisoma mitandaoni na unajiuliza je, zinafanya kazi ama ni kupoteza muda tu?

Habari njema ni kwamba baadhi ya tiba hizo zimethibitishwa kwa njia za kisayansi kwamba zinafanya kazi .

Imebainika wazi sasa kwamba kuna mimea na mazao yanayotokana na miti mbali mbali yenye viungo vyenye tiba na hapa tunakupakulia baadhi ya tiba hizi za nyumbani unazoweza kuzitegema .

Pilipili kutibu maumivu

Pilipili ina kiungo ambacho kina umuhimu mkubwa wa tiba tangu jadi na sasa matumizi yake yameanza kukubalika na wengi sio tu kupitia chakula lakini pia kama dawa .
Ina kiungo kijulikanacho kama capsaicin ambacho kinatumiwa kuweza kudhibiti maumivu ama uchungu .Inafanya kazi kwa kuwasha sehemu ya ngozi kwa kuipa joto na ukali kabla ya kufikisha ganzi baadaye .

Leo unaweza kuandikiwa dozi ya apsaicin kwa jina Qutenza ambayo inatumiwa sana kudhibiti uchungu.

Jitengezee Krimu ya capsaicin na mafuta ya nazi

1. Changanya vijiko 3 vidogo vya poda ya cayenne na kikombe 1 cha mafuta ya nazi.

2.Pasha moto mafuta kwa joto la wastani hadi iyeyuke.

3.Koroga mchanganganyiko huo kwa dakika 5.

4.Ondoa kuoka motoni kisha ipoe na kuweza kuganda.

5.Jikande kwenye ngozi baada ya kupoa.

6.Ili kuifanya nyororo ongeza mafuta ya nazi uweze kutumia vizuri kwenye ngozi bila kujikwaza .

7. Ni vizuri kufanya majaribio ya athari zake kwa ngozi yake kabla ya kuitumia kikamilifu .

Usiitumie krimu hii karibu na uso au macho yako na hakikisha unavalia glavu kabla ya kujipaka unapotaka kupata afueni

Tangawizi kutibu maumivu na kichefuchefu
Ni kama ada kutumia tangawizi ukijipata na mafua au koo lako linakoroma na matumizi yake sio ya kubahatisha kwani imebainika kwamba tiba hii inafanya kazi na ina uwezo mkubwa sana wa kukupa afueni.

Pia chai ya tangawizi itakusaidia kuzuia kuhisi kichefuchefu. Kuitengeza dawa ya tangawizi ni rahisi kama kusukutua kwani unachohitaji ni kuiponda ama kuitumia iliyosagwa na kuitumia katika chai.

Tangawizi pia ina viungo vya kutuliza maumivu na mara nyingi hata dawa za homa na mafua zimetegezwa kwa baadhi ya viungo vya tangawizi .

Uyoga wa Shiitake kuzuia kansa ya matiti
Lentinan, al maarufu kama AHCC ni kiungo kinachotoka kwenye uyoga wa Shiitake ambaco huzua uvimbe wa seli na husaidia kabisa mchipuko wa uvimbe unaoweza kusbabisha kansa .

Iwapo utafurahishwa na supu ya mifupa wakati unapoitumia basi usisahau kutupa ndani aina hii ya uyoga ili kuiboresha tiba hiyo hata Zaidi .

Mafuta ya Mikaratusi/ Eucalyptus kupunguza uchungu
Aina tofauti ya mmea wa Mafuta ya Mikaratusi

Mafuta ya mikaratusi yana kiungo kwa jina 1,8-cineole, ambacho kupunguza uchungu.

Kiungo hicho kina athari kama ya morphine na kimefantywa uchunguzi na kugunduliwa kuwa na uwezo mkubwa wa kukupa afueni unapopitia maumivu.

Hata hivyo matumizi ya mafuta ya eucalyptus sio ya kila mtu .Mafuta haya yanaweza kuchochea Asthma na pia kudhuru wanyama wa nyumbani .

Lavender kuumwa na kichwa na uchovu
Maumivu ya kichwa wakati mwengine yanaweza kukuathiri ghafla bila kuwa na dawa za kupunguza makali yake

Iwapo utakumbwa na maumivu haya basi usichelee endapo una lavender au majani yake.

Pia tiba hii ya nyumbani husaidia kupunguza uchovu na matatizo ya kifikira endapo umechoka kupindukia

Mnanaa/Mint kwa maumivu ya misuli
Mint, inajulikana na wengi na ina manufaa mengi ikiwemo kufungua mkondo wa kupumua iwapo umesakamwa au hata kupunguza maumivu ya misuli .

Kwa uchungu wa misuli tafuta yenye kiungo cha methyl salicylate, iliyo na athari ya capsaicin. Kuitumia kutakupa hisia kama ya 'kuchomwa' na inapooza.

Aina nyingine ya mint inayotumika sana ni peppermint. Kiungo hiki kinatumika sana kutibu maradhi ya koo au kutoa fueni wakati unapokabwa na mafua .

Kando na matatizo ya tumbo mafuta ya peppermint au chai ya peppermint inaweza kusaidia kupunguza maumivu ya kichwa .

Vyakula vyenye Magnesium kwa kila kitu
Iwapo kuna kiungo kinachoweza kukupa afueni ya matatizo mengi nyumbani basi ni vyakula vyote vyenye madini ya magnesium.

Iwapo utapatwa na matatizo kama uchovu, kuumwa na kichwa na maumivu ya misuli basi tiba hii ya nyumbani itakupa afueni .

Mboga na matunda yenye magnesium ni kama Spinachi, avocado, na hata chokolati nyeusi .

Vyakula vyenye magnesium
•Maharagwe ,mbaazi
•tofu
•Nafaka
•samaki wa mafuta kama chache
•Ndizi

Hakikisha unazitumia ifaavyo tiba za nyumbani
Ingawaje nyingi ya tiba hizi hazina madhara ya pembeni kunazo zenye athari kama hizo zikitumiwa kwa wingi kupindukia.

Watu wengine huenda wakajipata mashakani kwa kupitisha kiasi cha tiba hizo na wakati wote unafaa kufahamu kiasi na njia ifaayo ya kuitumia tiba yoyote kati ya hizi .

Iwapo mwili wako haustahimili matumizi ya vitu kama protini basi pia kuwa mwangalifu na uepuke tiba zenye viungo vya protini .

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post