WATANZANIA WATAKIWA KUJENGA TABIA YA KUFANYA MAZOEZI

Na Woinde Shizza ,Dodoma

Mganga mkuu wa Serikali Profesa Abel Makubi amewataka wananchi kujenga tabia ya kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha kinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza pamoja na yale yasiyo ya kuambukizwa.

Ameyasema hayo leo wakati akiongoza mazoezi ya pamoja akiwa na watumishi wenzake kutoka Wizara ya Afya ,ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa pamoja na wananchi wa jiji la Dodoma mazoezi yalifanyika katika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma.

Alisema kuwa wananchi wengi wamekuwa na mazoea ya kukaa bila kufanya mazoezi jambo ambalo linawasababishia kushambuliwa na magonjwa mara kwa mara.

"Mazoezi yanasaidia sana kuondoa magonjwa yasiyoambukiza kama sukari na presha ,pia huondoa usongo wa mawazo pamoja na kuleta mahusiano baina ya kundi na kundi ,mtu na mtu au na jamii nzima na muunganiko wa kazi kupitia mazoezi hayo",alibainisha Makubi.

Aidha mbali na kufanya mazoezi mganga mkuu wa Serikali pia alishiriki katika zoezi la uhamasisha wananchi kufanya usafi kwa kushiriki zoezi la kufanya usafi wa mazingira katika uwanja wa Nyerere Square.

Akiongea wakati wa kufanya usafi huo amewataka wananchi kuimarisha usafi wa mazingira ili kujikinga na magonjwa ya kuambukiza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post