NYAMAGANA WAFANYA SHEREHE KUWAPONGEZA WALIMU KWA MATOKEO MAZURI SHULE ZA MSINGI


Diwani wa kata ya Nyamagana  Bhiku Kotecha akionyesha tuzo ya pongezi kutoka ofisi ya Rais  TAMISEMI baada ya kata hiyo kuwa mshindi wa kwanza Kiwilaya katika mtihani wa kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka 2020


Na Hellen Mtereko Mwanza

Hafla ya kuwapongeza walimu kwa matokeo mazuri kwa shule za msingi zilizopo kata ya Nyamagana Mkoani Mwanza imefanyika leo Februari 19,2021 katika viwanja vya shule ya msingi Nyamagana.

Hafla hiyo imelenga kuwapongeza walimu hao kwa juhudi zao za kuimarisha ufaulu kwa Wanafunzi wanaohitimu darasa la Saba.

Akizungumza katika hafla hiyo Diwani wa kata hiyo Bhiku Kotecha alisema kuwa matokeo mazuri kwa wanafunzi hutokana na ushirikiano ikiwemo kufanya kazi kwa bidii kwa walimu wote.

Alisema kuwa nidhamu nzuri katika maeneo ya kazi ni njia moja wapo ya kuleta chachu ya maendeleo ya kielimu katika shule husika.

Aidha Kotecha alitoa mifuko miwili ya sukari yenye ujazo wa kilogramu 25 katika shule ya msingi Nyamagana kama zawadi ya kuwapongeza walimu.

Mkuu wa shule ya msingi Nyamagana, Anadoreen Rugaimukamu alisema kuwa kati ya shule zilizoko kwenye kata 18 wilayani Nyamagana kata ya Nyamagana imekuwa ya kwanza na imetoa mwanafunzi Bora wa kwanza wa kiume katika ngazi ya wilaya.

Alisema ushindi huo umetokana na ushirikiano mzuri waliokuwa nao Kati ya Walimu na Wazazi katika suala zima la kutambua umuhimu wa masomo pamoja na malezi bora.

Rugaimukamu alitoa wito kwa Wazazi na Walezi kuwa watambue vipaji vya watoto wao ili waweze kujikita kwenye hicho kitu anachopenda mtoto kwani kwakufanya hivyo itasaidia kutimiza ndoto zao.

Jelly George ni mwanafunzi aliyehitimu darasa la Saba katika Shule ya Msingi Nyamagana mwaka 2020 na alifanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika ngazi ya Wilaya.

Alisema siri ya mafanikio yake alikuwa anawasikiliza walimu kwa umakini kwakile walichokuwa wakifundisha darasani na Kama kitu hajakielewa alikuwa akimfata mwalimu kwa muda wake ili amfundishe tena.

Jelly kwa Sasa anasoma Shule ya sekondari Ipwaga iliyoko Wilayani Misungwi Jijini Mwanza na ana ndoto za kuwa daktari wa Moyo hivyo anasoma kwa bidii ili aweze kutimiza ndoto yake.


Kwa upande wake Baba mzazi wa Jelly Yusuph Yahaya alisema kuwa nidhamu nzuri waliyomfunza tangu akiwa mdogo imesaidia kwa kiasi kikubwa kufanya vizuri kwenye masomo yake.
Diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha akizungumza kwenye hafla ya kuwapongeza Walimu wa kata hiyo kwakufaurisha Wanafunzi vizuri.
Diwani wa kata ya pamba Bhiku Kotecha akizungumza kwenye hafla.
Diwani wa kata ya Nyamagana Bhiku Kotecha akikabidhi mfuko wa sukari kwa mwalimu
Jelly George mwanafunzi aliye anya vizuri kwenye matokeo ya darasa la Saba 2020 na kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza kiwilaya
Baba mzazi wa Jelly,Yusuph Yahaya akizungumza ufaulu wa mwanae.
Anadoreen Rugaimukamu mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Nyamagana akifanya mahojiano na waandishi waa habari katika viwanja vya Shule hiyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post