RAIS MAGUFULI ATOA KAULI WALIOMZUSHIA KIFO WAZIRI WA FEDHA DK. MPANGO..ASOMA SMS MSIBANI ....ATAKA TUSITISHANE

Rais Magufuli na Waziri wa Fedha. Dk Mpango (kulia)

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli amekanusha taarifa za uzushi zilizosambazwa mtandaoni kuwa Waziri wa Fedha Dk. Philip Mpango kuwa amefariki dunia na kuwataka Watanzania kuachana kuogopeshana na kutishana na wachukue tahadhari dhidi ya Ugonjwa wa Corona   huku wakiomba Mwenyezi Mungu.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ijumaa Februari 19,2021 wakati akiongoza waombolezaji kuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

"Imefikia mahali sasa tunatishana sana. Leo asubuhi nilitumiwa Meseji na Waziri wa Fedha Dk. Mpango ambaye amelazwa Dodoma na ninaomba niiosome hapa kwa faida ya wale waliokuwa wana Twitt kwamba amekufa",amesema Rais Magufuli.

Rais Magufuli amesema katika SMS hiyo, Dkt. Mpango amemueleza Rais Magufuli kuwa kwa Neema ya Mungu anaendelea vizuri, anakula vizuri na anaendelea kufanya mazoezi ya kifua na kutembea na kwamba wale waliomzushia mtandaoni kuwa amefariki dunia amewaombea kwa Yesu wakati wa Sala ya Jioni jana.

Ujumbe wa Maandishi uliotumwa na Waziri wa Afya kwa Rais Magufuli unasomeka ifuatavyo:

"Mheshimiwa Rais asante sana nimepata ujumbe wako kupitia kwa mke wangu. Kwa Neema ya Mungu ninaendelea vizuri,ninakula, ninafanya mazoezi ya kifua na kutembea. Hao wanaonizushua kifo kwenye mitandao niliwaombea Msamaha kwa Yesu wakati wa sala ya jioni jana. Mheshimiwa Rais Mungu akubariki na akupe Neema na ujasiri zaidi katika kuliongoza taifa letu katika wimbi hili. Naungana nawe na familia katika maombolezo ya kifo cha mpendwa wetu, Mhe. Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi. R.I.P".

Rais Magufuli amesema magonjwa yapo na yataendelea kuwepo hivyo kuwataka Watanzania kuendelea kuchukua tahadhari huku wakimuomba Mungu.

"Nitachotaka kuwaambia ndugu ni kwamba Magojwa yapo na yataendelea kuwepo, magonjwa ya vifua, magonjwa ya kupumua na kadhalika yatakuwepo na hayakuanzia hapa, Zipo Nchi ambazo zimepoteza watu wake wengi. Sisi Tanzania Mungu ametusaidia sana mwaka uliopita, tuendelee kuchukua tahadhari huku tukimuomba Mungu. Mungu Hashindwi".

Naomba tusitegemee nguvu za ubinadamu, bali tumtegemee Mungu. Narudia ndugu zangu tujue Mungu yupo. Mungu ndiyo muweza wa yote. Nashukuru viongozi wa dini mmeendelea kulihubiri hilo. Tuendelee ndugu zangu kusimama na Mungu. Tulishinda mwaka jana, inawezakana hili ni jaribu jingine, nalo tukisimama na Mungu tutashinda",  amesema Rais Magufuli.

Tusitishane na kuogopeshana, tutashindwa kufika. Inawezekana kuna mahali tumemkosea Mungu. Inawezeakana kuna mahali tunapata jaribu kama wana wa Israel walivyokuwa wanaenda Kaanani. Tusimame na Mungu ndugu zangu Watanzania. Kufa tutakufa tu,unaweza kufa kwa malaria,ukafa kwa Kansa,ukafa kwa magonjwa mengine kwa sababu kufa kupo lakini Kamwe tusimuache Mungu",amesema Rais Magufuli. Huo ndiyo wito wangu", amesema Rais Magufuli.

"Tusimame na Mungu ndugu zetu Waislamu walitangaza muda wao wa kuomba na niliambiwa na Mufti,niwaombe tena Watanzania kama kuna mahali tumetereka tuendelee kumuomba Mungu. Tuanze leo kwa ndugu zetu Waislamu,kesho Jumamosi kwa ndugu zetu Wasabato wanaosali Jumamosi na Jumapili kwa ndugu zetu Wakristo kwa kumuomba kufunga kwa siku tatu. Mimi nina uhakika tutashinda. Nataka niwape nguvu hiyo ndugu zangu Watanzania",.

"Naomba Viongozi wa dini muendelee kusisitiza maombi. Tulishinda mwaka jana, tutashinda mwaka huu, tutashinda miaka yote kwa sababu kamwe Mungu hajaweza kuliacha taifa hili.Tumeshinda mwaka jana na tukaingia kwenye uchumi wa kati na Corona ipo,uchumi ukaendelea kupanda na Corona ipo,miradi ikaendelea kutekelezwa wala hatukuweka Lockdown hata sasa hatutaweka Lockdown kwa sababu tunajua Mungu yupo siku zote. Taifa hili lipo mikononi mwa Mungu",amesema Rais Magufuli.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post