Picha : MVUA YA MAWE NA UPEPO YALETA MAFURIKO SHINYANGA MJINI...IBINZAMATA, KITANGIRI WAPATA TABU


Muonekano wa mafuriko katika daraja la Kitangiri - Ibinzamata Mjini Shinyanga

Na Kadama Malunde- Malunde 1 blog

Mvua iliyoambatana na mawe iliyonyesha kwa takribani dakika 45 kuanzia saa tisa alasiri leo Jumamosi Februari 13,2021 Mjini Shinyanga imesababisha mafuriko na kukata mawasiliano katika baadhi ya maeneo likiwemo eneo la kutoka Ibinzamata kwenda Kitangiri.

Maeneo mengine yaliyoathirika ni Mtaa wa Viwandani, Mnara wa Voda na maeneo ya masoko ambapo maji yameririka kwa wingi kuingia kwenye nyumba za watu yakiwemo maeneo ya biashara na kusababisha uharibifu wa mali mbalimbali.

Malunde 1 blog imefika katika eneo la vivuko/madaraja ya kutoka Ibinzamata kwenda Kitangiri ambapo wananchi wameonekana wakihangaika kuvuka na wengine wakilalamika vibanda vyao kusombwa na maji.

Wananchi wamesema mafuriko hayo yamesababishwa na miundombinu mibovu ya barabara ambapo kuna madaraja na makalavati madogo yaliyoharibika pamoja na mitaro kuziba hivyo kusababisha maji yashindwe kupita.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga, David Nkulila amesema tatizo la mafuriko katika manispaa hiyo linasababishwa na ubovu wa miundombinu ikiwemo mitaro na makalavati ya kupitishia maji akibainisha kuwa maeneo yaliyoathirika zaidi ni maeneo yenye tatizo la mito.

 “Hii Mvua imekuja kwa kasi hatukuitarajia, imenyesha kwa muda mfupi ikiwa imeambatana na upepo na kusababisha maji kufurika na kufunika madaraja na maji kuingia kwenye nyumba za watu”,amesema Nkulila.

Wananchi wakivuka kutoka Kitangiri kwenda Ibinzamata na wengine kutoka Ibinzamata kwenda Kitangiri. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mwanamke akivuka eneo la daraja/kivuko kutoka Kitangiri kwenda Ibinzamata 
Vibanda vikiwa vimezingirwa maji katika eneo la Ibinzamata
Wananchi wakitafakari kuvuka kutoka Ibinzamata kwenda Kitangiri
Wananchi wakiendelea kuvuka katika eneo la Ibinzamata
Wananchi wakiendelea kuvuka katika daraja la pili kutoka Ibinzamata kwenda Kitangiri
Mwananchi akitafakari kuvuka katika daraja la pili/kivuko cha pili kutoka Ibinzamata kwenda Kitangiri
Wananchi wakitafakari kuvuka au la!!!
Wananchi wakiendelea kuvuka
Maji yakiwa yamezingira nyumba eneo la Kitangiri
Mwendesha bodaboda akimvusha mama na watoto wake katika daraja/kivuko cha Ibinzamata kwenda Kitangiri
Mwendesha bodaboda akimvusha mama na watoto wake katika daraja/kivuko cha Ibinzamata kwenda Kitangiri
Hapa ni katika eneo la Mnara wa Voda wafanyabiashara wakiendelea kuondoa maji ndani ya vyumba vyao vya biashara

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments